Tangazo : Unahitajika msaada kufanikisha utafiti na ripoti kuhusu ualbino Tanzania
Jana nilipomaliza kuposti habari ya machungu yangu juu ya dhuluma dhidi ya albino, nilipata ombi kuhusiana na habari hilo, ombi ambalo nililishughulikia kadiri ya uwezo binafsi kupitia marafiki waandishi wa habari ninaofahamiana nao. Tayari jana iyo hiyo nilipata majibu ya matumaini kuwa huenda mawasiliano na dada Vicky Ntetema wa BBC yakapatikana. BBC imeripoti kwa kina kuhusu dhuluma hii, bofya kusikiliza visa vyenyewe kwa KiSwahili na English.
Leo nimepata wazo jingine. Ninaomba msaada kwa yeyote anayeweza kufikisha ombi la kumpata Mwanshidi wa Habari ama mtu yeyote mwenye kuweza kusaidia kufanikisha kazi na utafiti unaokusudia katika kufahamu chanzo na pengine suluhisho la kupambana na dhuluma hii kubwa dhidi la albino.
Hili limekuwa doa na aibu kubwa katika historia ya ukatili kwa binadamu, sioni sababu ya kuendelea kulisemea kimya kimya wakati wageni wanafika katika nchi yetu na kupeleka taarifa hizi mbaya. Tumeficha tende, mguu ukatunga usaha na sasa umetumbuka tunanuka sote. Ni kweli wahenga waliposema kuwa, 'mficha maradhi, mwishowe kifo kitamuumbua'. Hatuna cha kuficha tena, tafadhali tutumie fursa zote zilizopo ili tuushinde uovu huu. Kama ni kutangazwa vibaya kama ile documentary ya Mapanki, basi na iwe hivyo, kwa kuwa wanapokufa albino tayari ni sifa mbaya kuliko sifa mbaya nyingine yoyote.
Ninayo anwani, mawasiliano ya simu na anwani ya makazi [physical address] ya mwandishi na mwanahistoria huyu wa taaluma ya utafitii wa mambo ya kale (anthropology). Yeye amefanya shughuli zake nyingi kama 'anthropologist' katika nchi za Africa na anazo ripoti kadhaa zinazopatikana kwenye mtandao kuhusiana na: witchcraft, rumors and rituals murders in africa. Katika mojawapo ya mawasiliano yetu nilimwuuliza maswali kadhaa na alinitumia baadhi ya ripoti ndefu [detailed report] ya kazi zake. Sehemu ya majibu ya baadhi ya majibizano yetu inasomeka hivi:

Yes, I just came back from Mali and Sénégal. I'm a former anthropologist, and I have worked in West Africa also in Namibia, Malawi, Mozambique, Angola, Congo, Madagascar...Ikiwa unataka kuacha maoni yako na maelekezo kupitia kisanduku chamaoni ni sawa kwakuwa nitayakopi na kumtumia.
I plan to travel to Tanzania [in the lake region] this summer but I need to find a driver with car (4X4) and a translator English - Swahili...
2 feedback :
sDada Sibira. Sijui ni vipi watu wanaweza kukubaliana nami na sina haja ya kukubaliana na aliye na mtazamo hasi. Lakini naamini kwa wenye mtazamo chanya watakubaliana nawe kuwa katika kusaka habari endelevu, elimu endelevu, changamoto za kuboresha namna tunavyoielimisha jamii na namna ya kuiwezesha kuondokana na UMASKINI na KUJIKOMBOA KATIKA UTUMWA WA KIAKILI, wewe ni SHUJAA WETU.
sNasema haya nikimaanisha na japo sijaacha maoni na maelekezo ya kufanikisha hili, napenda kusema CHANGAMOTO YETU BLOG inathamini saaaaana mchango wako kwa jamii yetu.
s Nami nitasaka na kufikiria ninaloweza kufanya kufanikisha kusaidia hili na nitatenda kwa kadri ya uwezo wangu.
s HESHIMA KWAKO, KAZI NJEMA NA MAISHA MEMA SAAANA
s
s NB: Naomba usishukuru maana sisi twashukuru kwa kazi zako na shukrani yako ni kuendeleza utendayo maana ni faida kwa jamii yetu.
s
Mube ushasema nisiongee, haya, nimeuchuna.
Nafurahi kuwa mawasiliano na da Viky yamewezekana na huenda mambo yakaenda sawwa tukapata habari pia toka kwa mtafiti wa mambo ya kale kuhusiana na imani za kishirikina na uchawi.
Shukrani kwenu mliosaidia hasa timu ya BBC Swahili.