wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, November 22, 2008

TweetThis! Si sahihi kuua! Hasa ikiwa ni mwanadamu - tena albino!

Upumbavu wa baadhi ya watu Tanzania!

Unaweza kurejea kwa kubofya hapa ili usome  nicholiandika hapo awali kuhusu ualbino.
Katika siku za hivi karibuni vimekuwa vikiripotiwa visa vya kutisha juu ya mauaji, tena yale mauaji ya kikatili kwa binadamu wenzetu ati tu kwa kuwa ngozi zao za rangi ya tofauti. Vyema ukidhani kuwa, binadamu asiridhike kwa hali za maisha alizo nazo, lakini, isipitilize! We mtu anadiriki na kuthubutu kufanya ukatili alimaradi ajitajirishe ama kupata mali hata ikiwa mali hizo zitatokana na kumuua binadamu mwingine! Ati vyovyote viwavyo, alimradi atimize tamaa zake! Kwa aliye mwamini atakubaliana na Mfalme Sulemani kuwa pamoja na kupata utajiri wote alioutamani hapa duniani, kwa hekima za juu kuliko binadamu wote alizopewa na Mwenyezi Mungu, Nabii Sulemani anasema katika kitabu cha Mhubiri na Mithali ya kuwa "...yote hayo nayo ni ubatili mtupu sawa na kujilisha upepo". Ufahari katika maisha ya mpito hapa duniani si mali kitu jamani.

Pamoja na kuwa nilisoma na kuzisikia kwa juu juu habari za mauaji ya albino, kwa kweli sehemu ya kwanza kabisa iliyolivalia njuga katika fani ya uandishi wa habari na kuliripoti vilivyo suala hili ilikuwa ni kupitia BBC (bofya kutizama video fupi) katika kipindi cha Dira ya Dunia alichoripoti bi Vicky Ntetema, hata kufikia kutishiwa maisha. Tokea hapo nimesikia habari hii ikiripotiwa kwenye redio nyingi zaidi, blogu televisheni na hata magazetini.

Dhana potofu kabisa ya mauaji ya albino inatokana na imani zilizoshamiri za kichawi na kishirikina ambazo nimeziandika mara kadhaa (kisa cha kwanza na kisa cha pili). Siku zote jamii ya watu wasioelimika ni rahisi sana kuamini kwenye upotofu. Aghalabu, imetokea hata walioelimika kujihusisha na imani potofu kama tulivyosikia vituko vya wabunge na hata baadhi ya wasomi katika maofisi fulani fulani wakifanya vitendo vyenye dhana ya kishirikina (sheria ya uchawi). Wanasbabisha tujiulize na kutia kasoro katika maana halisi ya kuelimika!

Woga na wasiwasi huambatana zaidi na vitendo vya kishirikina na uchawi. Na woga husababisha mtu akatenda jambo ambalo asingethubutu hata kuliwaza angelikuwapo na utimamu wa kiakili.

Hii ndiyo hasa hali inayosababisha ndugu zetu kuuawa bila sababu za msingi bali kutokana na ujinga na kufilisika kimawazo kwa baadhi ya watu fedhuli.

Laiti ingekuwa ni kupiga kura kuchagua baina ya makundi kupata kujua ni kundi lipi linalohitaji ulinzi wa hali ya juu, basi albino wanapaswa kuwa namba moja katika makundi yote kuliko kitu kingine chochote!
  • Kigezo chake cha kwanza ni kwa uwa kilichomo hatarini kwa watu hawa ni uhai wao ambao kila mtu aliye hai ametunukiwa na Mola mara moja tu bila malipo yoyote.
  • Kigezo cha pili ni kwa kuwa binadamu hawa tayari wanayo mengi ya kuyakabili maishani kutokana na mapungufu katika miili yao, wanahitaji kupendwa ili kupunguza na kuondoa kabisa unyanyapaa wanakumbana nao katika jamii isiyowapokea kwa usawa.
Iweje leo watu wengine wajigawie amri, mamlana na uwezo juu ya kuwepo ama kutokuwepo kwa uhai wa mtu mwingine pasina maelezo ya kina zaidi ya uchawi na ushirikina ambao siku zote umekuwa ukiharibu na kubomoa maisha?

Thamani ya uhai wa mtu ni utajiri kiasi gani? Utajiri na mali ya kufaa kwa maisha gani hadi udiriki kuua mtu?

Itakuwaje pale ambapo watu wengine watadai uhalali wa uhai wako na ukashindwa kuutetea uhai wako wewe mwenyewe?

Na, kutokana na kisomo nilichoandika hapo awali ikatokea maishani mwako ukapata 'vitiligo', je! utajihalalisha kuuawa ili kuwapa wengine faida ya utajiri wa dunia hii unaopita?

Hapa nimerekodi baadhi ya vipindi vilivyorushwa na BBC kuhusu mauaji ya kutisha ya albino.

Sikiliza kisa kilichotokea Kigoma:


Sikiliza kisa kilichotokea Mwanza :

1 feedback :

ruhuwiko said... Sat Nov 22, 07:45:00 AM MST  

kwa kweli inasikitisha sana na pia inaogopesha sha. Katika Tanzania yetu yenye amani hivi watu wanawaza nini na nani aliwaambia eti ngozi hiyo ni mali sana. kama si ni kukosa akili nini. et nikiweka hii dukani au nyavuni basi nitafanikiwa nani kasama hilo

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads