wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, November 08, 2008

TweetThis! Dhana ya uchawi na vitendo vya kichawi kisa cha pili

Wakati fulani tuliwahi kusikia kisa cha kutisha na kusikisisha kilichotokea eneo la Tabata mjini Dar es Salaam, ambapo mtoto-mtuhumiwa alikamatwa katika eneo la hospitali ya Muhimbili akiwa na mfuko wenye kichwa cha binadamu (mtoto mdogo wa kadiri ya miaka mitatu hivi). Mtuhimiwa alipohojiwa kutoa maelezo alisema kuwa alikuwa akipeleka 'nyama' kwa shangazi yake ambaye ni mmoja wa wafanyakazi waajiriwa wa hospitali hiyo.

Kutokana na kisa hicho, watu wengi walichangia na kutoa maoni tofauti.

Kundi moja la baadhi ya watu walidai kuwa hilo ni tatizo la kisaikolojia na kuwa si dhana ya uchawi hasa ikizingatiwa kuwa mtoto mtuhimiwa anayedaiwa kutenda kosa hilo aliwahi kukubwa na mkasa wa kudaiwa kuanguka katika Kanisa la Mikocheni TAG.

Kundi jingine walitahadharisha kuwa uchawi na vitendo vya kichawi ni vya kweli na hutokea katika maisha ya kila siku hivyo kila mmoja anapaswa kuchukua tahadhari kwa kumrejea Muumba kwa toba, sala na maombi.

Kundi la tatu ni lile la watu wasiosimamia upande wowote bali kutokujali sana kuhusu habari za uchawi na kuona kama vile ni jambo la kupita tu.

Jana nilisikia habari kupitia redio ya BBC Swahili inayoelezea kisa cha mama kwa jina Adelina Elias, wa kijiji cha Ngara, mkoani Kagera aliyekuwa anakiri kurithishwa uchawi kutoka kwa wazazi wake akiwa na umri wa miaka kumi na tano tu na kuendelea na vitendo vya kichawi. Katika mahojiano hayo, anasema kuwa uchawi upo na ameutumikia na kwa sasa amechoshwa anaachana na vitendo vya uchawi na kumrudia Mungu.

Je! Uchawi ni dhana inayoambatana na ukosefu wa elimu na wingi wa fikira na imani potofu ama inawezekana kabisa kuwa hata aliyeelimika dhana ya uchawi bado ni hai? Nauliza hivi kwa kuwa nimekutana na watu walioelimika kwa misingi ya dunia hii lakini imani za kichawi ni dhahiri katika akili zao na huwa wamejaa hofu ya uchawi! Inasikitisha!

Sikiliza kisa hiki nilichokirekodi kutoka Dira ya BBC Swahili bofya kifute (Novemba 7, 2008)

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads