wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, March 25, 2009

TweetThis! Ijue na itumie RSS kutuma au kupokea habari

RSS ni njia mojawapo rahisi ya kupashana habari baina ya msomaji wa blogu/tovuti na mwenye blogu/tovuti ni kwa njia ya RSS. Hii ni njia mahsusi hasa kwa watu ambao kwa sababu zisizozuilika hawawezi kutembelea blogu/tovuti husika kila mara. Vile vile ni njia rahisi kuwafikishia wasomaji habari mpya.
Ukiwa katika blogu ya nukta77, tafuta picha/icon zilizooneshwa hapa kisha zibofye ili uweze kujichagulia namna unavyopenda kupokea habari.
  RSS (Realy Simple Syndication) au XML (eXtensible Markup Language) ni njia ya kuwasilisha posti za blogu/tovuti kwa wasomaji/watembeaji bila ya kuwalazimu kufika kwenye blogu/tovuti yako.
  Subscribe ni wito wa kutaka ujiandikishe kupokea habari/posti mpya za tovuti/blogu hiyo.
  Kisoma habari (Feed Reader / RSS aggregator) hutumika kukuletea habari ulizojiandikisha kupitia RSS.

  Mahsusi kwa wasomaji wa blogu:
  Kila mara unapotembelea tovuti yenye RSS ni rahisi kuona mojawapo ya alama inayofanana na hiyo inayoonekana hapo kushoto ama maandishi yanayosomeka "Subscribe". Ili kupokea habari za blogu/tovuti hiyo unapaswa ku-bofya alama hiyo au maandishi hayo, kisha utapata uchaguzi wa kisoma habari na namna ya kupokea posti mpya za blogu/tovuti uliyoitembelea. Mifano ya njia hizo ni kama inavyoonekana kwenye picha na unachotakiwa kufanya ni kufungua akaunti na kisoma habari unachokipendelea. Ikiwa mwenye tovuti/blogu atakuwa amesahau kuweka utambulisho wa kuonesha kuwa tovuti/blogu yake ina RSS, baadhi ya visoma habari vinaweza kung'amua ikiwa tovuti/blogu hiyo ina RSS pale utakapoibandika linki ya tovuti/blogu unayotaka kuifuatilia. Orodha ya visoma habari inapatikana hapa (bofya).

  Mahsusi kwa wenye blogu/tovuti:
  • Jinsi ambavyo ungependa habari ziwafikie wasomaji wako kupitia RSS feed itategemea na uchaguzi wako. Hii ina maana, unaweza kuchagua ikiwa wasomaji watumiwe posti nzima ama sehemu tu ya posti hiyo na kisha wamalize kusoma posti nzima kwa kubofya linki itakayofungua kwenye blogu/tovuti yako.
  • Ili kuwafikia wasomaji wengi na kuwapunguzia usumbufu wa kufungua kila posti na kusubiri ukurasa wa blogu yako kufunguka, ni vyema ukawatumia posti nzima (Full Feed).
  • Blogger ina huduma ya RSS feed by default kwa kila blogu. Ikiwa unatumia Firefox browser ama Opera utaona alama ya yenye rangi ya machungwa au bluu sehemu ya address bar upande wa kulia. Bofya alama hizo ili kuona chaguzi zilizoko na pia kupata linki ya feed ya blogu/tovuti husika. Ikiwa unatumia IE ama browser ambayo haina uwezo wa kufahamisha ikiwa tovuti inayo ama haina RSS, basi wasaidie wasomaji wako kwa kuweka widget (element) za 'Subscribe' ambapo watapata uchaguzi wa kujiandikisha kwenye aidha 'Posts' au 'Comments'. (tizama picha hapo kushoto kuona mfano).
  Hii hapa ni video inayoelezea RSS kwa lugha ya kiingereza.

  0 feedback :

  Recent Comments . Kauli za Wasomaji

  ###recentComment###

  More Opportunities ads