wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, November 15, 2008

TweetThis! Uwanja wa Fisi: Maisha ya Eliza

MPYA: Soma marejeo baada ya filamu.

Hii ni filamu inayosimulia maisha ya Eliza Joseph.
Eliza alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu tu alipokata shauri na kufunga safari kuelekea mjini. Kama walivyo watoto na vijana wengi waishio mikoani, Eliza aliamini ahadi na ndoto ya kusomeshwa na hatimaye kujipatia ajira atakapofika huko mjini.
Waimbaji waliasa:
Mjini shule.
Mjini chuo kikuu.
Mjini shule.
Mjini ndiyo mambo yote.
Akiwa na umri wa miaka kumi na tano tu, Eliza alibakwa na mwajiri wake! Kisa hiki kiliishia kwa yeye kuswekwa lupango. La haula la kwata!

Hatimaye maisha hayakuwa maisha tena kwa Eliza. Ili kujikimu kwa mahitaji ya kila siku, Eliza ilimbidi kuishi maisha ya umalaya katika Uwanja wa Fisi, eneo maarufu mjini Dar Es Salaam. Alitumia madawa ya kulevya kujiliwaza na kusahau machungu aliyoyapata. Alikata tamaa. Hatimaye Eliza aliambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na Virusi vya UKIMWI.

Ama kweli maisha ni safari ndefu iliyojaa misukosuko, shida na chembechembe ndogo za raha!

Msomaji wangu, tizama video ili kujua hali ya Eliza ilivyo leo hii.
Na hiki ndicho kisa cha Eliza...

AU

Filamu imetengenezwa kwa udhamini wa Maweni Farm
AU


Eliza Joseph came to town when she was thirteen, following promises for a job and the possibility to go to school. At the age of fifteen she had already been raped by her employer and stayed three months in prison. She ended up as a sex worker in Dar es Saalaam's infamous Uwanja wa Fisi (Hyena Square). Today she saves other girls from that life. More at hyenasquare.org

POST REVISIT:
Read here the interview by Cecilia Bäcklander
Meet the interviewer, photographer and film maker here

MAREJEO 1
Picha za Eliza zinapatikana WomenOnTheRun, BongoCelebrity na TanzaniaAffairs

MAREJEO 2
Kutokana na usumbufu wa baadhi  ya wasomaji kushindwa kutizama filamu hii, nimeipakua na kuibebesha kwenye tovuti ya kusafirisha mafaili makubwa. Tafadhali bofya hapa (badongo) au  hapa (filesavr) au Hapa (divshare) kujipakulia nakala yako.
Filamu hii itumike kwa madhumuni ya kuelimisha jamii na si kwa kujipatia faida iwayo yote ile.

Zingatio:

1 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads