Kufanya kazi Marekani : Wauguzi [updated]
Habari hii inamhusu yeyote anayehitaji kufahamu utaratibu wa kufuata ili kufanikiwa kufanya kazi nchini Marekani kama RN/Nurse/Muuguzi/Nesi jinsi inavyoelekezwa katika tovuti ya Serikali ya Marekani. RN ni nani? tovuti hiyo inafananua, soma "Registered Nurses"
Ninafahamu njia mbili ambazo nitazielezea hapa. Kabla hujachagua ni njia ga ni uifuate, huna budi kujua kuwa njia zote zinakuhitaji uwe:
- Umesoma na kufika katika kiwango cha shahada ya uuguzi (Degree of Nursing holder).
- Na leseni hai ya Uuguzi inayokubalika katika ngazi za kimataifa mf. Leseni iliyotolewa na inayotambulika na chama cha wauguzi Tanzania nk.
Njia ya Kwanza: Fuata maelekezo kwa kujiandikisha katika tovuti ya Commission on Graduates of Foreign Nursing Schools® : (CGFNS)
1. Utatakiwa kufungua anwani ya barua pepe (bure) katika tovuti ya CGFNS ambayo wataitumia kukufahamisha maendeleo ya kila kinachofanyika na ulichofanya katika maombi utakayowatumia.
2. Utatumiwa ama unaweza kupakua fomu toka kwenye tovuti hiyo. Fomu hizi zina maelekezo yanayojitosheleza ya nini cha kufanya. Kwa ufupi, fomu moja utatakiwa kujaza maelezo yako na kisha kuwatumia CGFNS, fomu ya pili utatakiwa kuipeleka katika chuo ulichosomea shahada ya Uuguzi, wataijaza na kuipiga muhuri kisha hakikisha wanaituma CGFNS, fomu ya tatu utatakiwa kuipeleka Wizara ya Afya kwenye kitengo kinachohusika na Wauguzi ambapo wataijaza na kuipiga muhuri, vilevile hakikisha nayo wanaituma CGFNS.
3.Utatakiwa kulipia gharama za kushughulikia tathmini ya kiwango chako cha elimu ikilinganishwa na kile cha Marekani kupitia Credentials Evaluation Services. Hapa watachambua elimu yako na kuidhinisha endapo ina kiwango sawa na cha Muuguzi aliyesomea Marekani. Jinsi ya kulipia, utatakiwa kufuata utaratibu waliouweka wao.
4. Endapo CGFNS watathibitisha kuwa elimu yako ina kiwango kinachokubalika Marekani, utatakiwa kuchagua tarehe na mahali pa kufanyia mtihani wa awali yaani Certificaion Program Qualifying Exam, (CP) maelekezo ya ziada yanapatikana hapa: Requirements for the Certification Exam.
5. Ni jukumu lako kufuatilia kwa kupiga simu na kuulizia hatua iliyofikiwa katika kushughulikia maswala yako kwani, maombi yanayotumwa CGFNS ni mengi mno toka pande zote za dunia. Unatakiwa kufanya mtihani wa Kiingereza. Wakati unajiandikisha kwa mtihani huo, ni lazima uwajulishe kuwa majibu yako yatumwe na wao moja kwa moja CGFNS na namba ya kituo cha CGNFS. Unao uchaguzi kati ya mitihani miwili ya Kiingereza ambayo unaweza kufanya na ambayo inakubalika CGFNS, nayo ni aidha TOEFL ama IELTS. Maelezo haya pia yanapatikana kwenye tovuti ya CGFNS. Ukiwa Dar es Salaam, ninadhani unaweza kujiandikisha kwa mtihani wa TOEFL pale Mlimani, Chuo Kikuu kitengo cha Kompyuta (UCC) ama unaweza kupata maelezo pale Hilton Learning Center iliyopo Kinondoni - Mwembeni, inatizamana na jengo la Hugo. Kwa mtihani wa IELTS maelezo yanapatikana katika ofisi za British Council.
6. Ukifashafanya mtihani wa CP, endapo umefaulu, utatumiwa barua na cheti toka CGFNS inayokuruhusu kutafuta mwajiri katika nchi ya Marekani ambaye atatakiwa kukutumia barua ya ajira ambayo utaitumia kuombea VIZA katika Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ili upewe VIZA ya kukuruhusu kufanya kazi nchini Marekani.
7. Utakapofika Marekani, utatakiwa kufanya hatua ya mwisho ambayo ni kujiandaa kwa mtih ani wa kupata leseni ya kufanyia kazi nchini Marekani, mtihani huo unajulikana kama NCLEX. Maelezo na utaratibu wa jinsi ya kujiandikisha kwa mtihani wa NCLEX yanapatikana kwenye tovuti ya National Council of State Board of Nursing (NCSBN)
Njia ya pili: Njia hii unaweza kuitumia kwa ajili ya kufanya mtihani wa NCLEX moja kwa moja unaokuwezesha kupata leseni ya kufanya kazi nchini Marekani kama RN bila kufanya mtihani wa CP-CGFNS .
Njia hii itafanikiwa tu endapo:
- Unauhakika ama umeshapata VIZA yoyote ilenitakayokuwezesha kuingia nchini Marekani
- Umeshafanya na kukamilisha utaratibu ulioelekezwa katika namba 1-6 katika maelezo ha po juu.
- Umeshatuma maombi katika bodi ya Uuguzi katika Jimbo la Marekani unalotarajia kufanya kazi na kujibiwa endapo wanaruhusu kufanya mtihani wa NCLEX moja kwa moja bila kufanya mtihani wa CP-CGFNS. Jimbo la California, Arizona na machache mengineyo yanatoa uhuru kwa njia hii, kuhusu majimbo mengine ya Marekani, unahitaji kusoma maelek ezo katika fomu zao. Bodi hizo zinapatikana National Council of State Board of Nursing (NCSBN).
- Utakapofaulu mtihani wa NCLEX ukiwa nchini Marekani, utatakiwa kutafuta Mwajiri nchini humo atakayekuwa tayari kushughulikia utaratibu wa kukupatia kibali cha kazi na kubadili aina ya visa uliyojia ili kupata visa ya kazi ama "Kadi ya Kijani" = Green Card. Hakikisha kuwa unafanya mtihani wa NCLEX mapema kabla ruhusa yako ya kuwepo ndani ya Marekani haijaisha (kama una ruhusa ya miezi 6, hakikisha umejiandikisha kufanya mtihani miezi 4 kabla ya muda kwisha kwani utaratibu huchukua muda mrefu kwa wewe kutumiwa majibu unayoyahitaji sana katika kuanza taratibu za Uhamiaji).
Angalizo: Mitihani mingi ya Marekani haifuati mfumo wa mitihani ya Uingereza tuliyozoea kuandika majibu ya kujieleza mfano: short answers ama essays. Mithiani ya Marekani mingi ama karibu yote ya fani zote ni ya uchaguzi yaani "Multiple Choices Questions" (MCQ) ambayo ni migumu na ya kukanganya akili. Hawahitaji jibu sahihi tu, bali jibu sahihi zaidi.
Usisahau: Fanya maandalizi kwa kujiandikisha katika vituo vya kujipiga msasa kama vile Kaplan (wana madarasa unayoweza kuhudhuria ana kwa ana (ukiwa nchini Marekani) ama kujisomea kwenye mtandao (uki wa nje ama ndani ya Marekani). Pia wana benki ya maswali (Q-bank) unayoweza kuyatumia kujifua. Pia, tumia Google.com kutafuta zaidi juu ya CGFNS na NCLEX lakini kuwa macho na majambazi, wezi, wadanganyifu, wababaishaji, walaghai, n.k. wa mtandaoni wanaojidai wanafahamu sana kuhusu mitihani hii na habari za uhamiaji nchini Marekani. Kama unajiamini kuwa unaweza kujisomea peke yako, basi, nunua vitabu vya maandalizi na ujisomee kwa muda walao wa miezi miwili kwa juhudi.
Orodha ya tovuti za vitengo vinavyoshughulika na Uuguzi katika majimbo ya Marekani inapatikana katika tovuti ya NCSBN.
Contacting CGFNS/ICHP:
(to check status): (215) 599-6200 24 hours a day; 7 days a week Requires CGFNS ID Number & Date of Birth
Applicant Inquiries: (215) 349-8767*
Business Office: (215) 222-8454*
*Hours of operation: Monday through Thursday: 9:00 am to 5:00 pm (USA Eastern Time) Friday: 9:00 am to 4:30 pm (USA Eastern Time)
Ukitaka kujua majira katika majimbo ya Marekani ili ufahamu wakati gani muafaka kupiga simu, tafadhali bofya Time Temperature ama Time
Maelezo ya ziada ya wapi na jinsi ya kujifua kwa mtihani wa NCLEX na ile ya Kiingereza, bofya hapa
Ikiwa nimesahau jambo na nikalikumbuka, basi nitaliongeza wakati ujao.
label: AcademicGuides , | P.U.G.U/HowTo... |
9 feedback :
You are doing a great work Subi. Thanks for all the opportunities placed here. Kazi nzuri sana, Ubarikiwe
Dada SUBI wewe ni mtu wa ajabu na unastahili sifa, sijawahi kuona mtanzania kama wewe, wengi ni wa majungu na wifi, mungu akubariki na akuzidishie, ingawa mimi si muuguzi lakini nimefurahishwa sana na juhudi zako, haya mambo ndo yanayotakiwa watanzania wasaidiane. KEEP IT UP DON'T STOP UNTIL WATANZANIA WOTE WAONDOKANE NA UMASIKINI.
Yours,
EDWARD ALEX MKWLELE - edwardmkwelele@yahoo.co.uk
Asanteni sana kwa kunipa moyo na kufurahia nilichofanya.
Nitaendelea kuandika kadiri nitakavyojaaliwa kupata uzoefu ama kufahamu mapya zaidi.
Shukrani.
Subi,Naingia mwaka wa Kwanza kuchukua Nursing (diploma) nikimaliza nitakutafuta.
Kwa kweli haya ndiyo matumizi ya Mitandao siyo kufanya mambo ya ajabu yasiyo mpendeza Mungu.Nimefurahishwa sana na juhudi hizi unazo fanya kwani kweli wengi hupenda kwenda ng'ambo lakini nasema,"Hayo tutafanya Mungu akitujalia" wala si kwa mapenzi yangu.Ni mfano wa kuigwa na kama kila mtu ambaye Mungu amemjalia kuwa na mzingo na wengine angefanya kama Mungu anavyo kusudia Tanzania ingekuwa nchi ya ajabu sana.Lakini kwa sababu ya Ubinafsi na kujijali mtu mwenyewe mwenyewe hali ndiyo hiyo.Lakini Mungu si Athmani wala si Abdallah tutafika maana anasema,"Hakutuweka kwa hasira yake".
Keep up the good work Subi. Your light shines in the darkness. Thanks for the info.
Muuguzi chipukizi
Kwakweli dada Subi Mungu azidi kukupigania na kukuongezea kila inapoitwa leo. Ingawa habari zako nyiingi nilizijua kutoka ulipokuwa unafundisha muhimbili Nursing,wengi wanakusifia saana. Hebu tujitahidi tuwavute wauguzi wenzetu toka Tanzania na ninaamini hii retrogression ikiisha basi watakuja weengi saana.Nimeweza kuhudhuria Kaplani na Ready to pass woote niwazuri ndo najiandaa kufanya october.Kwakweli inabore saana maswali yao niyakuchagua yanachanganya saana.
Ninafurahi kusikia kuwa wapo wanaothubutu kujaribu na kupiga hatua! Inatia moyo sana. Asanteni kwa kutoa maoni, inanikumbusha ku-update hizi posti kila mara!
P.U.G.U
Hii wengi wanaijua ila ni wangapi wanaitekeleza?
Mmoja wa wachache ni wewe Da Subi.
THANKS