wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, July 14, 2009

TweetThis! Simu inaita toka Ubungo Maziwa, natumai ujumbe umefika!

Hii habari ya kukurupuka na kusema hili jema, ooh, hili zuri, ooh, hili lina faida bila ya kuwaelewesha wananchi na bila ya kujibu maswali yao, nasema ipo siku tutatafutana hapa nchini na vyanzo vya kutafutana vitakuwa hivi hivi mnavyovidharau.

Kila siku mna mkakati mpya na mbinu mpya za kutatua matatizo ya wananchi japo hamwashirikishi na mkiwashirikisha mnatumia shuruti ya kuwalazimisha wakubaliane na matakwa yenu. Kwa bahati mbaya sana, baadhi ya maamuzi mnayoyoyafikia na kuamua kuyatekeleza kabla ya kupima kwa kina faida na hasara, mmekuja kugundua kuwa yana madhara zaidi ya faida. Inapofika hatua kama hiyo, tayari uharibifu unakuwa umetendeka na inayobaki hapo tena ni kila mmoja wenu ninyi kushika njia yake na kubaki kuwaongopea wananchi kuwa, 'tunalishughulikia', hiyo kauli yenu hiyo siku moja wananchi wataitumia kwa vitendo kukuelekeeni ninyi, 'watawashughulikia'. Naomba siku hiyo isifike, mbona mtajuuuta!

beep tu -- triing, triing. alo, aloo!
Kero za wananchi wa Ubungo Maziwa
Picha kazipiga braza Mroki mwenye blogu ya MrokiM

1 feedback :

Mzee wa Changamoto said... Tue Jul 14, 06:18:00 PM MST  

Serikali yetu ina wimbo mzuuri kuwa kiila kitu KINASHUGHULIKIWA. Nasubiri wananchi watakapoanza kuwashughulikia hawa walio madarakani.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads