wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, July 14, 2009

TweetThis! Mwalimu Mwakasege aonya udini chini

Habari imeandikwa na Charles Mwakipesile katika gazeti tando la Majira
Mhubiri wa Kimataifa, Mwalimu Christopher Mwakasege amewaonya Watanzania kuacha mawazo ya Tanzania kuongozwa kwa sheria za kidini.

Mwalimu Mwakasege alitoa rai hiyo juzi wakati akifundisha katika semina ya siku ya nane ya neno la Mungu katika viwanja vya Barafu Mjini Dodoma na kusema matatizo yanayoikabili nchi hayawezi kutatuliwa sheria pekee bali kumtanguliza Mungu.

Alisema wakati malumbano mbali mbali yakiwa yanaendelea ni vema Watanzania wakafahamu kuwa suluhisho la matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi yanaweza kumalizwa kwa maombi.

Mwalimu Mwakasege alisema, tabia ya kufanya maombi ya zima moto kamwe hayawezi kuwa ukombozi wa matatizo maombi ya kuzama ndani zaidi.

Mtumishi huyo wa Mungu aliwataka Watanzania kuanza utaratibu wa kufanya maombi makubwa kuanzia ngazi ya kitongozi hati Taifa kuiombea Tanzania na mambo mabaya yanayoinyemelea.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads