wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, July 20, 2009

TweetThis! Kampuni Tanzania inatafuta mshirika wa utengenezaji gesi ya katani

Kampuni ya Segera Estates inatarajiwa kujikika katika shughuli za utengenezaji wa gesi asilia (biogas) kutokana na mabaki ya mmea wa katani.
Kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake Afrika ya Kati na Mashariki imefikia uamuzi huo baada ya kupata mafanikio katika majaribio madogo iliyofanya kwenye mradi wake wa mashamba yaliyopo Hale na Korogwe mkoani Tanga. Kampuni hii kwa sasa inatafuta mshirika ambaye wataongeza juhudi katika kulifanikisha hili.

Kampuni nyingine binafsi ijulikanayo kwa jina, Katani, imethibitisha kuwa mradi huu wa uzalishaji gesi asilia kutokana na mabaki ya mmea wa katani inawezekana kwani, katika mradi ambao ulifunguliwa rasmi mwaka jana na Raisi wa Tanzania mhe. J. Kikwete alifungua rasmi alipokuwa mkoani Tanga, tayari umezalisha kiwango cha kilowati 150 za umeme kinachoweza kutumika katika shughuli za mashine kwa saa 12 mfululizo. Kampuni ya Katani tayari imeshafungua kampuni ndogo kwa jina Mkonge Energy System ambayo itatengeneza nishati ya umeme kwa ajili ya biashara kutoka kwenye mabaki ya mkonge na vitu vingine vinavyoweza kutengeneza nishati ya umeme.

Huenda gesi hii ikasaidia kuongeza uwezo wa upatikanaji nishati ya umeme na kupunguza utegemezi wa aina moja tu ya nishati, yaani ile inayotegemea maji ya mvua. Vile vile gesi asilia *inaweza kuwa njia mojawapo ya utunzaji mazingira*. Inaaminiwa kuwa, matumizi ya gezi asilia hupunguza kiwango cha gesi yenye madhara, yaani Methane, na gesi zinazotokana na 'green house' (na sijui kwa nini wakaziita green hizi zenye kuleta madhara kwenye hali ya hewa kiasi kikubwa namna hii, zinazalisha hasara kubwa bora wangeziita red houses au jina jingine, eniwei, ndo maisha).

2 feedback :

Anonymous said... Wed Sep 02, 05:04:00 AM MST  

Sijaelewa hapo Mwanzo,Kampuni ya Segera Estate?hiyo statement inaweza ikaleta maana tofauti kabisa unamaanisha kweli kuna Kampuni inaitwa Segera Estate?maana ninavyojua mimi kuna Kampuni inaitwa SAGERA ESTATE na Sio SEGERA ESTATE na hiyo Sagera haiusiani na Katani Ltd kabisaa ni wadau wawili tofauti katika Sector ya Mkonge..,na wanao deal na maswala ya Energy kwa uwelewa wangu ni Katani Ltd na si Sagera na katani ndio waliofungua Kampuni ya MKONGE ENERGY SYSTEM na ndio wenye kiwanja Cha umeme Mkonge kilichopo Hale.Asante

Subi said... Wed Sep 02, 05:38:00 AM MST  

Anonymous,
Asante kwa maoni yako.
Habari ilikusanywa kutoka linki hizi:
1. http://tinyurl.com/kp9pmm
2. http://tinyurl.com/n3j4cu
3. http://tinyurl.com/n3j4cu
4. http://tinyurl.com/ktraen
Hata na hivyo, inawezekana kabisa ikawa jina ndilo tu limekosewa kutokana na kuzoeleka kwa jina la Segera zaidi ya Sagera na hasa kwa kuzingatia eneo linalozungumziwa na linavyohusika na kilimo cha mkonge na uzalishaji katani.
Asante.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads