Richmond haikulipwa hata senti 5 - Waziri Simba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Bi. Sophia Simba, amesema suala la kufikishwa mahakamani watuhumiwa wa Richmond bado lina utata kwani kampuni hiyo haikulipwa hata senti tano.
Kauli hiyo ya Waziri Simba ni mpya na inatofautiana na taarifa zote zilizowahi kutolewa kuhusu kampuni hiyo hadi kusabisha kuvunjwa mkataba wake huku baadhi ya mawaziri akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, kujiuzulu kutokana na utata katika mkataba wake na gharama za uendeshaji.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Simanjiro Bw. Christopher Ole Sendeka bungeni jana, Waziri Simba alisema watuhumiwa wa EPA na IPTL wanashughulikiwa kisheria na kwamba hawezi kujibu lolote kuhusu hatma yao kwa kuwa anakatazwa na Sheria za nchi.
“Nadhani Mheshimiwa Mbunge anatambua kwamba Serikali inafuatilia kwa karibu masuala hayo na EPA ipo mahakamaini, siwezi kuzungumzia lolote, suala la Richmond ipo katika hatua mbalimbali na lina utata kwa kuwa haijalipwa hata senti tano," alidai Bi. Simba na kusababisha wabunge wengi kuguna.
Katika swali lake la nyonge, Bw.Sendeka aliitaka Serikali kuchukua hatua za utashi wa kisiasa kwa kuwachukulia hatua za haraka watuhumiwa wa Richmond, EPA na IPTL ili kuweka nchi katika sura nzuri ya kupambana na rushwa - Majira.
0 feedback :