wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, June 10, 2009

TweetThis! Mbinu mpya za wizi wa kompyuta

Kisa hiki kimetokea kweli kwa mkazi wa Dar. Nimeweka hapa kwa ajili ya kuwatahadharisha tu. Shukrani za pekee zimfikie aliyekumbwa na mkasa na kuamua kutufahamisha kwa tahadhari.


Salamu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo!

Wapendwa naomba niwasimulie yaliyonipata siku ya tarehe 4/6 siku ya Alhamis katika maeneo ya masaki barabara ya kahama majira ya saa 1:15 jioni, ambapo gari ndogo aina ya saloon iliponipita na kusimama mbele yangu, nikafikiri ni mtu anayenifahamu, nilipoifikia ile gani nikapita,ikiwa na watu wawili yaani dreva na mwingine akiwa amekaa nyuma na dreva akajifanya anaongea kwenye simu.

Nilipopita hatua kama kumi ile gari ikaja nyuma yangu na kunipitia karibu sana kwa mwendo wa taratibu, nilipostuka tayari yule aliyekaa nyuma akakamata begi yangu ya Laptop na kuivuta, tukaburuzana nikijaribu kuinusulu komputa yangu na dreva akaongeza speed, huku naburuzika ndipo nikashindwa nguvu na kuachia, nikaanguka chini na kuchunika magoti na mikono huku suruali ikiwa haivaliki tena. Pamoja na laptop wakachukuwa kitambulisho changu chs chuo, driving licence kitambulisho cha kupigia kura,flash disk 2 na kadi ya uanachama wa NSSF.

Wapendwa nimeshea nanyi wizi huu ili kwamba tuwe makini na wizi wa namna hii ambao mimi sikuwaza kabisa kuibiwa kwa namna hiyo.

Vile vile naomba sana maombi yenu kwani nimepoteza document zangu muhimu sana kwa shule yangu, ikiwemo research proposal yangu ambayo sikuisevu penginepo popote.

AHSANTENI SANA.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads