wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, May 20, 2009

TweetThis! Raisi wangu kaenda zake Marekani kuwaombea watoto hawa kompyuta nini?

Posti iliyopita ulimwona Raisi wangu akitembelea ofisi za Google zenye limashine likubwa na mawaya kibao, sasa mi nadhani alikwenda kuwaombea watoto hawa (pichani) kompyuta. Kaka Rwebangira wa BongoPicha amewanasa hivi watoto wa darasa la saba katika shule ya msingi Maendeleo (ndiyo, maendeleo, sijui kuelekea wapi) huko Mbagala, wenyewe wanafanya mtihani wa moku (mock). Baba, Mheshimiwa, Raisi wangu eeh, tafadhali rudi na zawadi kemkem na za kutosheleza, si utizame tu mwenyewe kwenye picha? unadhani natania? si kujifanyisha hii, walahi tena kweli imetokea!
 
 

1 feedback :

Malkiory said... Wed May 20, 12:48:00 PM MST  

Kwa mwendo huu ile programu ya komputa kwa kila mwanafunzi ina maana yeyote chini kwetu, kama mambo yenyewe yako hivi. Inasikitisha kwa kweli, wakati hali kama hii ikiendelea kuwatafuna wanafunzi wetu, hivi karibuni waziri mkuu amewaambia wabunge kuwa anatarajia kuboresha maslahi ya wabunge!

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads