wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, May 20, 2009

TweetThis! Raisi wangu yupo zake Marekani

Picha iliyopigwa kwenye ofisi za Google huko Silicon Valley, San Jose, [inatamkwa Hosee] Marekani inamwonesha raisi wangu akipewa elimu huku akitolea mimacho hiyo midude yenye njia za panya. mmhhh, raisi wangu we, ya kweli hayo? Kweli kweli kabisaaa? Si utani! mwe!
Natumai wapo watu wa TeknoHaMa wameambatana an raisi na sijui ni kwa kiwango gani watanasa habari, eniwei, raisi wangu ananiacha mbali sana kwa safari zake il hali ameteua na kuwapa madaraka wawakilishi wake katika nchi hizo. Utendaji kazi wa nchi tajiri, raisi wake humsikii akiwa nje ya nchi yake kwa zaidi ya siku mbili, labda iwe na ulazima wa pekee, zitizame hizo nchi za Japan, Ujerumani, Urusi, Uingereza, Ufaransa nk nk, huku kwetu kwenye umasikini vile vile sijasikia safari za Vasco Da Gama toka kwa raisi Paul Kagame wa nchi ya Rwanda inayowika na kuja juu kwa kasi katika kukua kwa uchumi wake, wao nawaona wapo bize wanashughulika na watendaji wa ndani kuona ni kwa jinsi gani watautokomezea mbali umasikini wa wananchi wao na kuboresha maisha yao.
Inanishangaza kwa kweli, uongo si kazi. Ni mengi nisiyoyajua na hivi nabaki kushangaa tu. Labda ipo sababu nzuri na ya maana sana, mie nsiseme mno kama juha, kwanza sifahamu lolote kuhusu uongozi. Bora nkachume tembele zangu nisonge ugali wangu, nile, nikalale, ya kesho yana Mungu tena.

2 feedback :

EDWIN NDAKI (EDO) said... Wed May 20, 01:59:00 AM MST  

aaahaaa..aaa nina kajiharaka ila narudi nikupatia mawazo yangu..kuhusu maswali mawili matatu uliojiuliza..wewe wakati unawahi kuchuma matembele maana ndio jua la utosi ngoja mimi niwapeleke ng'ombe wangu wakapate ze 'drinki' kwenye mito iliyokauka kutokana na wananchi kukataka sana kuni kwenye vyanzo vya maji ..na serikali imeshindwa kutoa mbadala wa nishati ..na kukalia semina za mionzi ya jua 'kempikisiki hoteli'

tutafika tu

malkiory said... Wed May 20, 12:40:00 PM MST  

Subi,

Mambo ya vacation hayo, wala usishangae. Hapo utakuta kaandamana na watu kibao ambao wanajihesabia night allowances, achilia mbali nauli na gharama zingine.

Usijali, hayo ndiyo mambo ya ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, na maisha bora kwa kila mtanzania.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads