wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, May 15, 2009

TweetThis! Niendelee kushiriki au nihame Kanisa?

Swali ulilosoma hapo juu ameliuliza Patrick kupitia blogu ya StrictlyGospel.
Kwa mchango na majibu kuhusiana na mada hii pamoja na nyingine nyingi, tafadhali fika kwa dada Mary D wa StrictlyGospel.wordpress.com uache maoni yako ili kumsaidia Patrick na wengineo kwa kuwa ndiko alikotuma dukuduku lake. Nimeiweka habari hii hapa ili kuongeza wingi wa wasomaji na kwa kuwa suala hili limekuwa chanzo kikuu cha baadhi ya watu kukerwa hadi kufikia kuhama nyumba za ibada, madhehebu na hata dini.
Naomba msaada wa ushauri. Karibu mwaka sasa nimekuwa naenda kanisa moja la Kipentekoste hapa jijini Dar. Pamoja na kwamba mahudhurio ya watu ni wengi na nyimbo nzuri zinaimbwa na watu wanaonekana kuomba kwa dhati mimi nikiwa ni mmojawapo. Lakini bado sina raha na hilo kanisa kiasi kwamba mara nyingi ikifika jumamosi huwa namwambia mke wangu jumapili hii tukasali kanisa lingine. Lakini jumapili ikiwadia tu basi hamu ya kwenda kanisa hili nililolizoea hunijia. Basi naenda. Sasa mambo yanayonikwaza ni haya yafuatayo:
1.Kama wewe ni mtu wa hadhi katika jamii (au ni tajiri na huwa unatoa fungu la kumi mara kwa mara),ukifika umechelewa wale wahudumiaji watakulazimisha ukakae kiti cha mbele hata kama kumejaa waliotangulia wanahamishiwa viti vingine. Jambo hili mimi naona linaenda kinyume na Yakobo 2:2-3.

2.Wapo baadhi ya wachungaji na wazee wa kanisa ambao ndoa zao zimejaa dosari na wengine wake zao wamewakimbia na Mchungaji Kiongozi anayajua hayo lakini bado wanatoa huduma pale kanisani na hata kushiriki kutoa mapepo na kuwaombea watu kwa kuwashika mikono. Iweje Kiongozi wetu hayakemei hayo? Huwa ninajiuliza. Je Biblia inasemaje kuhusu hayo? Haya mambo si yako kinyume na 1 Timotheo 3:8?

3. Ni dhahiri Kiongozi wetu wa kanisa anapenda fedha na anawavumilia waumini wenye fedha hata kama matendo yao ni kinyume. Akiona mwenye fedha au hadhi haonekani kanisani huwa anasononeka sana. Anapenda waje kanisani kwake kwa sababu mahubiri yake huonyeshwa kwenye Chanel 10 TV mara moja kwa juma hupendelea hao watu waonekane ili wawe chambo kwa watu wengine waanze kwenda kanisani kwake. Mwenyewe huyaita masangara yake. Kwa hiyo humuagiza mpiga picha ahakikishe hayo masangara yanaonekana na humwambia apige picha zaidi watu waliokaa mbele kwa sababu huwa wanakuwa ni wale vigogo ndani ya jamii akina baba na masuti yao na akina mama na malemba yao makubwa.

4. Kuna baadhi ya waumini pale ambao wamevunja ndoa za watu kwa ama mke kuchukuliwa na mume wa mtu wa kanisa lingine au mume kuchukua mke wa mtu mwingine. Na zipo ndoa ambazo zimefungishwa pale huku ikifahamika kuwa hawa wana waume au wake lakini hakemei. Sasa mimi nauliza inakuwaje?

5. Hili ni kanisa au ni Club? I am confused. Jamani nisaidieni.

Sasa ndugu zangu huku siyo kuendesha kanisa kibiashara? Hebu nipeni ushauri niendelee kushiriki au nihamie kanisa lingine?

–Patrick

3 feedback :

Anonymous said... Mon May 18, 09:10:00 AM MST  

mimi nakushauri ndugu yangu usihame, wewe endelea kusali hapo hapo na unapopata nafasi basi unaweza kuitumia kuwahubiria juu ya neno la Mungu.hata biblia imeeleza wazi pale ambapo imesema acha magugu na ngano yakue ila wakati wa mavuno magugu yataachwa na ngano zitavunwa. hakikisha unakuwa ngano katika kanisa hilo. kumbuka pia mfano wa wanawali kumi ambapo watano walikuwa werevu na watano wajinga. basi inawezekana hata huyo kiongozi wenu ni mwanamwali mpumbavu. wewe hakikisha nyendo zako ili bwana harusi afikapo taa yako iwe na mafuta na hao matajiri wataachwa nje. Mungu anaona yote hayo na atayaleta hukumuni kwa kuwaambia siwajui

Anonymous said... Tue May 19, 06:00:00 PM MST  

Nakubaliana na wote hapo juu, lakini nionavyo mimi ni kwamba huwezi kua kiroho na kuthibitika kiimani kama kila jpili unamadukuduku na uongozi wa kanisa. Kama unasikia rohoni kwamba unatakiwa ubaki ili usaidie basi baki au la hakuna hukumu yeyote kwako kwa kuongoka na kwenda mahali ambapo utastawiri na kukuwa kiroho. The problem of remaining is the development of the spirit of critism and cynicism is everything that is going on even genuine things, and it hurts you more than anybody else. I personally happened to be in that situation for more than 5 years and the best advise for you is its is better to quit in peace than in pieces!

Na kumbuka chochote unachosema nje juu ya uongozi kama huwaambii wahusika na mchungaji mwenyewe basi ni majungu na uzushi na nikinyume na adili ya Biblia

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads