wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, May 30, 2009

TweetThis! Michezo: Juma Kaseja, Maurice Sunguti na Gaudence Mwaikimba huru kujisajili na timu yoyote

KITENDO cha Kocha Mkuu wa Yanga, Dusan Kondic kumtema kipa wake, Juma Kaseja katika usajili wa kikosi chake msimu ujao, kimempa uhuru wa kujiunga na timu yoyote aitakayo.

Kaseja amekuwa akifanya siri kubwa ya kikosi atakachokichezea msimu ujao huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kujiunga na timu yake ya zamani ya Simba.

Kondic amekaririwa kuwatema wachezaji watatu, Maurice Sunguti na Gaudence Mwaikimba katika kikosi hicho akiwemo Kaseja kwa madai kuwa, pamoja na kusajiliwa kwa dau kubwa, lakini ameshindwa kuwatumikia ipasavyo mabingwa hao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseja alisema hana taarifa ya kutemwa katika kikosi hicho, lakini kama ni kweli hakuna tatizo kwake na atamshukuru kocha wake.

Alisema hana analojua katika hilo, lakini kama kocha ameamua kumtema hakuna shida kwani anasubiri kumaliza mkataba wake na Yanga ndipo atakapojua timu atakayojiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara.

"Mimi ndio kwanza nakusikia wewe, lakini kama kweli wamenitema katika usajili, hakuna shida kwani wao ndio walionifuata msimu uliopita, labda msimu huu wameona sifai, hakuna shida," alisema Kaseja.

Alisema pamoja na taarifa hizo, lakini bado ni mchezaji wa Yanga hadi Juni 6, mwaka huu ambapo atajua ni timu gani atakayoitumikia msimu ujao.

Taarifa zenye uhakika kutoka kwa watu wa karibu wa kipa huyo, zilisema kuwa, tayari amekamilisha mipango ya kujiunga na Simba na anachosubiri ni kumalizika kwa mkataba wake na Yanga.

Kondic aliwahi kusema kuwa, Kaseja anaweza kuondoka na kujiunga na timu yoyote anayotaka kwani hana ubora wa kutisha sana huku akitoa tathmini ya michezo aliyocheza na mabao aliyofungwa.

Pia, Kondic alidai ni bora kumsajili Ali Mustafa 'Bathez' wa Simba kuliko Kaseja na katika wachezaji wanane anaotarajiwa kuwasajili, kuna makipa wawili na mmoja kutoka ndani ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kumnasa kipa huyo - Majira

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads