wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, May 30, 2009

TweetThis! Mbunge wa Moshi Vijijini, Aloyce Kimaro anusurika kifo katika ajali

*Alitegeshewa mawe barabarani

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo wilayani Moshi vijijini, Aloyce Kimaro amenusurika kufa katika ajali mbaya baada ya gari alilokuwa akisafiria kuparamia mawe yaliyokuwa yametegwa barabarani.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanajrao, Bw. Lucas Ngh’oboko alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku katika eneo la kijiji cha Lembeni Mikongeni wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.Alisema Mbunge Kimaro akiwa na abiria wengine watatu katika gari lake lenye namba za usajili T340 AZL aina ya Mercedes Benz wakiwa safarini kutoka Dar es salaam walipofika maeneo hayo hawakuona mawe yaliyokuwa yametegwa barabarani na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

“Mheshimiwa Kimaro alikuwa safarini akitokea Dar kuja Moshi walipofika Mwanga ndipo gari liliparamia mawe yaliyotegwa barabarani na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi
ambapo gari lao liliharibiwa na mawe hayo upande wa mbele na tairi ya kulia kupasuka” alisema.

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mawe hayo yaliwekwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwa nia ya kuwapora watu ambao wangeparamia mawe hayo na kupata ajali hivyo kupora mali waathirika wa ajali hiyo.

Aidha alisema kwa kipindi cha nyuma eneo hilo lilikuwa na mfululizo wa matukio hayo ambapo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo waliweza kudhibiti
matukio hayo na kurejesha hali ya amani.

“Kwa tukio hili ni wazi kuwa suala la ujambazi limeibuka kwa kasi tutashirikiana na wananchi wa eneo hilo kuendesha operesheni maalum ya kukabiliana na matukio haya ili watu hawa wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria,” alisema. Hata hivyo kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi hao kutoa taarifa kwa viongozi wa
ngazi za wilaya na Mkoa zitakazo pelekea kukamatwa kwa wahalifu hao.

Wiki iliyopita Mbunge wa Kyela, Dkt Harrison Mwakyembe alinusurika kufa baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka baada ya kulipita lori. Baada ya ajali hiyo, polisi walimlaumu dereva kwamba alikuwa kwenye mwendo wa kasi na kwamba Dkt Mwakyembe alikuwa usingizini, huku Mbunge huyo akisisitiza kwamba kauli za polisi zenye zinampa wasiwasi kwamba huenda ajali hiyo ilipangwa.
Martha Fataely, Moshi - Majira

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads