wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, May 18, 2009

TweetThis! Hili ndilo jengo la shule ya kutoa kizazi cha ulimwengu wa kidigitali bwana!


Huu ni mfano wa hali ya mazingira ya shule zetu ambapo wanafunzi wanatakiwa wazingatie masomo, wafaulu kwa kiwango cha KiMataifa na waweze kupambana na mikiki mikiki ya karne ya 21!

Shangaa inakuwaje mwanafunzi wa Sekondari hajui kutumia kompyuta ama hajajifunza faida za kusoma kwa njia ya kompyuta. Jibu linafanana na swali, kuwa,
  • Itawezekana vipi katika mazingira kama haya ya kusomea?
  • Motisha itatoka wapi hapa?
  • Nadharia kwa vitendo inaendeshwaje hapa?
Maswali ni mengi kuliko majibu.
Hali inasikitisha na kukatisha tamaa.
Maisha bora kwa kila MTanzania! Ndiyo mzee!

Ni kweli kuwa si shule zote za Tanzania zipo katika hali hii na si ajabu shule kama hizi zipo chache sana, lakini bado haifuti udumavu ambao watoto wanaosomea katika shule hii wameupata. Kwa jamii inayojali raia wake wote, hakuna hata mtu mmoja anayestahili kupotea ati kwa kuwa wengi hawapotei basi akipotea mmoja au wachache si neno. Nafsi moja inapopotea ni gharama sawa sawa na kupoteza nafsi elfu moja kwani kila nafsi ina thamani isiyolinganishwa na nyingine! Tusihesabu wingi na idadi, tuhesabu ubinadamu.

Pichani ni Bweni la shue ya Sekondari Zingibari huko Mkinga linalohifadhi wanafunzi 25.
Alipolitembelea ghafla, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi bi Mwantumu Mahiza hakuweza kujizuia kutodondosha machozi.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads