wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, May 18, 2009

TweetThis! Embed comment box chini ya posti

Wakati fulani nilipata taabu nilipobadili template halafu ghafla nikapata kigugumizi jinsi ya kuweka comment box ionekane. Huwa napata shida sana kubofya blogu kisha ifungue 'pop up window' ndiyo niandike maoni au blogu nyingine ukitaka kuacha maoni basi ukibofya linki tu nayo inafunga ukurasa unaoutizama na kufungua ukurasa mwingine - kusema la haki hii huwa inanipunguzia apetaiti ya kuacha maoni. Ikiwa unakereka na wewe ni bloga, basi jaribu kubadili mfumo wa blogu yako kwa kutumia tip hii:

Njia ya Kwanza
Login kwenye blogger kama kawaida na ukiwa kwenye 'dashboard' bofya kifute cha 'settings' kisha bofya kifute cha 'comments'
Kwenye section ya tatu utaona maandishi kama yanayoonekana hapa:The embedded comment form can not be used if you have Post Pages disabled.

Hakikisha umechagua 'embedded below post'.
Nenda (scroll) hadi mwisho wa ukurasa kisha bofya 'save settings'
Sasa tizama blogu yako kama vile ambavyo atatizama msomaji wa blogu yako.
Ikiwa blogu yako ina code stahili, basi utaona comment box imefunguka chini ya posti husika (kama ilivyo kwenye blogu hii).

Njia ya Pili
Ikiwa blogu yako ina template ambayo haina code husika, basi rudi kwenye 'Dashboard' ya blogu yako, bofya kifute cha neno 'Layout' kisha bofya kifute cha 'Edit HTML' kisha bofya kwenye kiboksi cha 'expand widget template'

Kisha tafuta code hii:
<b:include data='post' name='comments'/>

Baada tu ya code hiyo, chini yake ibandike code hii:
<b:include data='post' name='comment-form'/>

Kisha nenda mwisho wa ukurasa na bofya 'save template'
Sasa fuata maelekezo ya Njia ya Kwanza niliyoeleza hapo juu.
Sasa tizama blogu yako kama ambavyo atatizama msomaji wa blogu yako.
Utaona comment box imefunguka chini ya posti husika.

Njia ya Tatu
Ikiwa njia ya kwanza na ya pili zimeshindikana, basi ipo njia ya tatu nayo ni:
rudi kwenye 'Dashboard' ya blogu yako, bofya kifute cha neno 'Layout' kisha bofya kifute cha 'Edit HTML' kisha bofya kwenye kiboksi cha 'expand widget template'


Kisha tafuta code hii:
<p class=’comment-footer’>
<a expr:
href=’data:post.addCommentUrl’
expr:onclick=’data:post.addCommentOnclick’>
<data:postCommentMsg/></a>
</p>
</b:if>

Iondoe code nzima na badala yake, bandika code hii:
<p class=’comment-footer’>
<b:if cond=’data:post.embedCommentForm’>
<b:include data=’post’ name=’comment-form’/>
<b:else/> <b:if cond=’data:post.allowComments’>
<a expr:
href=’data:post.addCommentUrl’
expr:onclick=’data:post.addCommentOnclick’>
<data:postCommentMsg/></a>
</b:if> </b:if> </p> </b:if>

Kisha nenda mwisho wa ukurasa na bofya 'save template'
Sasa fuata maelekezo ya Njia ya Kwanza niliyoeleza hapo juu.

Sasa tizama blogu yako kama ambavyo atatizama msomaji wa blogu yako.
Utaona comment box imefunguka chini ya posti husika.
Muhtasari:
  1. Blogu nyingi zina comment box chini ya posti 'by default' na mtu hahitaji kubadili chochote.
  2. Baadhi ya blogu inabidi kubofya kisehemu cha 'embed comment below post' (soma Njia ya Kwanza hapo juu).
  3. Baadhi ya blogu inakubidi kuongeza 'code' ili kuwezesha comment box kuonekana chini ya posti (soma Njia ya pili na ya Tatu).

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads