wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, May 20, 2009

TweetThis! Aliyebadili jinsi afariki dunia [English Version at the bottom]

Rafiki yangu mpendwa sana ananiandikia hivi:
Habari dada,
kama masaa 2 yaliyopita nilikuwa naongea na dada aliyejitambulisha kama dada wa huyu marehemu, anasema ni kweli aunt Victoria alibadili jinsia UK, na ana mchanganyiko wa Kingazija, Kichaga na Kihindi. Anahisiwa alikunywa sumu baada ya 'boyfriend' wake kuwa 'mwingi' kwa wadada wengine japo Vic alimpa 'boyfriend' gari aina ya 'Freelender' kama njia yakumweka karibu zaidi. Yawezekana ndugu zake walimtenga kutokana na hali yake ndo maana akajitambulisha kwamba hana ndugu akaomba akifa azikwe na yeyote. Jina la Victoria limetokana na bibi yake ambaye ni marehemu.
MGONJWA Victoria Armu aliyebadili jinsi amefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa baada ya kuhamishiwa akitokea Mwananyamala alikolazwa awali.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Muhimbili, Bw. Jezza Waziri, alisema hali ya marehemu ilianza kubadilika usiku wa kuamkia jana na kufariki saa moja asubuhi.

Aliongeza kuwa mwili wa Victoria umehifadhiwa chumba cha maiti hospitalini hapo kwani hadi anafariki,hakuna ndugu wala jamaa aliyejitokeza kumwona.

Bw. Waziri alieleza kuwa endapo ndugu wa mtu huyo anayesadikiwa kuwa mkazi wa Mbezi Beach, Dar es Salaam hawatajitokeza, taratibu za mazishi zitafanywa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Alisema vipimo mbalimbali vilivyochukuliwa kwa mgonjwa huyo tangu Hospitali ya Mwananyamala hadi alipolazwa Muhimbili,vinaonesha alikuwa akitumia dawa za kulevya.

Marehemu huyo alikuwa kivutio kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam baada ya kufikishwa Hospitali ya Mwananyamala na Polisi wa Kituo cha Kawe, Mei 17 saa 11 alfajiri ambapo ilidaiwa aliokotwa ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Mbezi Beach, akiwa hajitambui.

Baada ya kufikishwa hospitali,ulizuka utata wa kuandika jinsia yake,lakini uongozi uliamua alazwe wodi ya wanawake.

Hadi kfo chake ,madaktari hawakuruhusu waandishi wa habari kumwona wala kufanya mahojiano naye kwa maelezo kuwa kufanya hivyo ni kukiuka kiapo na maadili ya taaluma ya tiba.

Hata hivyo baadhi ya watu waliodai kumwona alipofikishwa hospitali siku ya kwanza, walisema Victoria alikuwa na sura ya kiume, mweupe akiwa ametoboa masikio na nywele zake zikiwa na asili ya kiasia huku matiti yake yakiwa yanaonekana kupandikizwa kwa kudungwa sindano.

Mmoja wa madaktari waliowahi kumhudumia wakati wa uhai wake, alidokeza kuwa marehemu huyo alioneka kubadili jinsi yake kutoka ya kiume kwenda ya kike miaka michache iliyopita na kupandikizwa viungo hivyo nje ya nchi.

Alidai alionekana kuwa alizoea kutembea na wanaume kwa muda mrefu kwa kutumia maumbile ya mbele na nyuma.

Moja ya mambo yenye utata hadi kifo chake ni pamoja na jina lake halisi ambalo hadi sasa inadaiwa anaitwa, Victoria Armu huku wengine wakidai anaitwa Abdallah Aluu.

Pia taarifa za baadhi ya watu wanaodai majirani zake, zilidai, marehemu hakuokotwa na Polisi bali alichukuliwa nyumbani kwake mtaa wa Kipongoso,Mbezi Beach baada ya kuzidiwa na kupiga kelele kuomba msaada. Mwenye nyumba alipiga simu Polisi, ndipo walikwenda kumchukua na kumpeleka Mwananyamala - Benjamin Masese, http://majira.co.tz
In English
Aunt Victoria of Mbezi Beach is dead. Born Abdala Aluu, Tanzania’s first public case of sex change from male to female anatomy, Aunt Victoria succumbed to possible slow poisoning at the Muhimbili National Hospital at 7.05am. Aunt Victoria was last Sunday rushed to Mwananyamala hospital in Dar es Salaam unconscious, due to what authorities then described as a suicide attempt, but Amminiel Aligaesha -- the hospital’s public relations officer – could only confirm the time of her death and that her body was preserved in the mortuary awaiting final legal opinion of her death (post-mortem).

The previous day, senior public relations officer Jeza Waziri had told the 'Daily News' that initial medical check-up had indicated that Aunt Victoria was found with traces of toxic drugs and exhibited symptoms of meningitis. At her residence, music from a radio set she had left playing before she was rushed to hospital on Mnday was the only sign of life – all else was sombre and somewhat eerie.

However, two men guarded at the gates to the unfinished casino, but both declined to disclose their identities on excuses that media had them confused – not knowing whether Aunt Victoria was dead or still alive. “So far we don’t have clear information about Aunt Victoria … the media are giving contradictory information about her health at Muhimbili,” one of them said.

Efforts to trace Mrs Urombo – the landlady and close confidant – proved futile. She reportedly found Aunt Victoria vomiting outside the rented facility last Sunday, and Aunt Victoria was said to be in great pain at the moment. One eyewitness who preferred anonymity said Mrs Urombo phoned police for assistance. “Police from Kawe came with two defenders and picked her,” he said. Aunt Victorias was constructing a casino at Banda Beach Club area that she intended to launch it at the end of this month.

Before changing her sex about ten years ago, Aunt Vick had married a European woman with whom he had two children. Emmanuel Petro, a neighbour of Mr Aluu’s at Mitimirefu during those days said he was a well respected family man – keeping cows, a job in which he employed a number of youths. According to these oral accounts, Mr Aluu separated with his wife upon his sex-change operation in China – having earlier sold off the family house. Until yesterday, not a single relative had turned up to claim her body for burial - http://www.dailynews.co.tz/home/?n=2022&cat=home

2 feedback :

Subi Nukta said... Thu May 21, 02:24:00 AM MST  

We Mwanasosholojia ebu urudi hapa tuelezee kabisaaa tuelewe hii sentensi yako hapo. Wacha kukimbia mbio mbio kama Edo Ndaki jana anasingizia ati anaenda kulisha mbuzi wake Engarenanyuki au sijui wapi huko hadi leo hajarudi...

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads