wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, May 21, 2009

TweetThis! Mwakyembe ajalini [updated] - yupo MOI

 
 
  • 18:37 AM Habari za hivi punde kabisa zinathibitisha kuwa Mhe. Mwakyembe amelazwa katika hospitali ya MOI - Dar es salaam kwa matibabu zaidi. Alisafirishwa kwa ndege toka Iringa hadi Dar.
  • Habari kamili isiyotofautiana na update iliyopiga unaweza pia kuisoma kwenye blogu ya kaka Beda Msimbe wa Lukwangule Ent.
  • 9:37 AM Taarifa za rafiki anasema kuwa Mhe. amezinduka na anafanyiwa uchunguzi na matibabu katika hospitali ya Mkoa, Iringa. Mheshimiwa alipoteza fahamu kutokana na mstuko wa ajali. Amepata majeraha katika taya (sina hakika upande gani).
9:12 AM: Taarifa zinadai kuwa Mhe. H. Mwakyembe amepata ajali huko Iringa na kuwa yu mahututi asiyeweza hata kuzungumza. Hii ni kwa mujibu wa kituo cha habari cha ITV. Mwenye taarifa za uhakika zaidi tafadhali?

2 feedback :

Anonymous said... Thu May 21, 06:22:00 AM MST  

Kwa nini aandamwe kila wakati kutaka kutoa roho ya kiongozi huyu shupavu?

Alitoka Kyela jana na inasemekana alipumzika Makambako jana usiku.Akadamka kuendela na safari yake Dar leo asubuhi. Baada ya muda kidogo dereva alianza kushindwa kuitawala gari barabarani na kisha ikagongana na lori. Inasemekana kulikuwa na watu wasiofahamika waliokuwa wakiifuata gari yake kutoka Kyela.Tairi la gari walau moja ya mbunge linasemekana lilichomoka katika ajali hiyo.

Wabongo mmeingiliwa, mko tayari kupambana na mafisadi? Mbunge huyu alijua hatari zote zilizopo kabla hajaanza vita hii.Kwa hulka yake hatishiki.Itakuwa aibu kama watanzania wengine watatishika baada ya tukio hili. Saa ya ukombozi imefika, mafanikio yapo jirani,vita si lelemama.

Mchezo mchafu au kukomaa kwa demokrasia na uhuru wa kujieleza? Mafisadi hawana hoja ila ujanja ujanja tu na mbinu za giza na chini chini.

ghaja said... Fri May 22, 02:00:00 AM MST  

Hata kama njama zimefanyika Mungu yupo pamoja naye kwani ni mmoja wa mashujaa aliyesimama imara katika kupambana na mafisadi ,Mungu atamlinda

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads