wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, April 21, 2009

TweetThis! DECI na kasheshe zake huko mitaani

Mgonjwa: Daktari naumwa sana moyo.

Daktari: Wewe ni mpenzi wa timu gani ya mpira wa miguu?

Mgonjwa: Kwa Tanzania mimi ni shabiki wa Simba na Ulaya mimi ni mpenzi Manchester United.

Daktari: Na unafanya kazi wapi?

Mgonjwa: Nilikuwa nafanya GTV, baada ya kufa nikapata kazi Paradise Hotel Bagamoyo.

Daktari: Una akiba yoyote ya fedha benki?

Mgonjwa: Ndiyo, akiba yangu yote ya fedha ipo DECI.

Daktari: Mmmh, unaishi wapi?

Mgonjwa: Naishi Kwembe wilayani Kinondoni.

Daktari: Subiri kufa maana hakuna tiba mbadala ya maradhi yako.

UFUNGUO:
  • Simba na ManU zilifanya vibaya katika mechi zake mwaka huu kiasi cha kuwapa huzuni mashabiki.
  • GTV ilikuwa ikirusha matangazo ya Tv ya Satelaiti na kufa ghafla huku wateja na wafanyakazi wakiachiwa hasara tupu.
  • Paradise Hotel ilipata ajali ya kuungua moto na kusababisha wafanyakazi wake kukosa ajira.
  • DECI ni mchezo wenye chembechembe ya upatu uliowasababishia hasara waliopanda mbegu zao baada ya Serikali kuupiga 'stop'.

Kwa nini ume"DECI' hela ya mboga?!
Credits: Kibwagizo cha maneno kimeandikwa katika blogu ya "SIMULIZI" ya Basil Msongo Picha kwa hisani ya E.Mtui wa kundi pepe la TAFESAssociates

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads