Jinsi ya kuweka 'Favicon' kwenye blogu
Rafiki yangu Mube majuzi ameniandikia kwenye 'comment box' kuwa ameona nimeweka hiyo alama ya .77 ambayo inaitwa 'favicon' kwenye blogu, nami kama kawaida ya blogu hii, kila ninapo P.U huwa nina G.U, hivyo leo nimeazimu kuelezea jinsi nililivyoiweka ili na wewe ukitaka upate kuweka.P.U.G.U. = Pata Ujuzi Gawia Umma (Kauli mbiu ya hayati Mwl. J.K. Nyerere)
Favicon ni sawa na ID ama utambulisho wa blogu au tovuti. Favicon huonekana kwenye address bar ya browser yako, mwanzoni tu kabla ya address link.
Faida za favicon ni sawa sawa na faida za kuwa na kitambulisho ama ID kwa kuwa zinamwezesha msomaji wa blogu kuwa na hakika na blogu aliyoifungua na vile vile kumpa urahisi wa kurejea pale ambapo mtu anakuwa amefungua zaidi ya tovuti moja hasa kwa wale wanaotumia tabbed browser (sijui kama bado kuna watu wanafungua windows nyingi za browser badala ya kutumia tabs). Bofya picha hapo kuikuza ili kuona mfano wa favicon.

- Tengeneza favicon kutoka kwenye picha ama kwa kutumia tarakimu. Mimi nilitumia Icon Generator niliyoipakua toka kwenye tovuti ya Adobe. Unaweza kupata kutengeneza favicon moja kwa moja kwenye mitandao kutoka kwenye picha. Uki-google utapata 'online favicon generators' tizama/chagua kwa kubofya hapa
- Ukishapata favicon itakubidi uibebeshe (upload) kwenye tovuti ya kuhifadhia picha, unaweza ku-google kama hizi hapa (bofya) ili upate linki ya kuunganisha.
- Sasa Login kwenye Blogger
- Ukiwa kwenye Dashboard, bofya neno Layout kisha bofya Edit HTML
- Tafuta code hii </title> na ukishaipata, BAADA yake, weka code hii:
<link href='URL linki ya favicon' rel='shortcut icon'/>
- Nenda kwenye tovuti uliyohifadhi favicon yako, kisha tafuta linki ya hiyo favicon. Kwenye tovuti nyingi inapatikana kwa kubofya picha na kisha copy maneno yote yaliyopo kwenye address bar ya browser yako, majina ya picha yanaishia na .jpg, .jpeg, .gif, .ico na kadhalika. Ukishaipata, rudi kwenye code uliyoiweka kisha ondoa maneno URL linki ya favicon na badala yake uweke linki ya favicon yako. Kuwa mwangalifu usijeondoa alama za kufungua na kufunga mabano yaani ' ' zinazoonekana kabla na baadaya maneno URL linki ya favicon.
- Bofya Save Template.
1 feedback :
Thanks for the PUGU.
Natafuta muda niweke zile tips zote, hii ya Favicon, ya ku-subscribe nk.Tupo pamoja daima dada.
MAKULILO Jr,
www.makulilo.blogspot.com