wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, March 12, 2009

TweetThis! Mbinu mpya za wizi Tanzania

Ujumbe huu umetumwa toka kwa rafiki.

Nimeonelea ni vema niwajulishe mbinu hii ya wizi ili muijue.

Kuna kijana ambaye anadai ametoka Morogoro na ametumwa na mzee wake kununua gari kumbe ni tapeli na mwizi.

Kwa kadiri ya wiki mbili kijana alikuwa akifuatilia Gari ambayo nilikuwa naiuza na nikaitangaza katika Dar - Advert . Alisema yakuwa yeye yuko Morogoro na anahitaji kuiona gari ; mnamo tarehe 25 /12/2008 asubuhi, tulipokea simu yakuwa tukutane na kijana ambaye ameondoka Morogoro tumuuzie hilo gari na mpigaji akiwa ni mzee wake kutoka Morogoro; baada ya muda kijana aliomba udhuru ya kuwa tarehe 25 ni Krismasi baba yake angependa aje kuangalia hilo gari ila yeye hataweza atafika tarehe 26/12/2008 .

Saa moja asubuhi tarehe 26/12/08 alipiga simu na tukaelewana tukutane naye B.P petrol station Mbezi Beach ..tulipokutana alicheki gari kama mnunuzi yeyote kutoka bodi mpaka engine.akaomba afanye road test -he is a good driver Alionyesha kuridhika na gari na kuonyesha nia ya kulipia fedha ambayo alikiri iko kwa jamaa ya baba yake aliyepo jmall ambaye ni agent wa oilcom.; alipotoka j mall alidai amepewa fedha ambayo ni dollar hivyo ilibidi tuende mlimani city kubadili fedha na kudeposit kwenye account kwani anasisitiza hapendi kulipana fedha mkononi angependa tulipane bank.

Tulipokuwa ndani ya bureau de change alikuwa akiwasiliana na jamaa zake na simu yake ilizima kwa kukosa chaji hivyo aliomba simu yangu kwa mawasiliano pia alielezea juu ya hali yake kuwa amekunywa dawa amoxyline na tumbo linamsumbua kwani hajapata kifungua kinywa hivyo angependa kwenda kuchukua maziwa hivyo alitoka nje huku akiwasiliana kwa kutumia
simu yangu.

Kwa vile nilishakaa naye kwa muda upatao masaa matatu na juu ya yote alikuwa ameacha bahasha yake ya dollars tulipokuwa tumekaa sikupata na wasiwasi naye kabisa. Alipotoka ndani tu katika dakika tano nilishuku hivyo nikafungua bahasha yake kuchungulia mzigo wa dolla nikakuta ni magazeti yaliyofungwa vizuri.

Haikuchukua dakika kumi watu ambao contact zao zilikuwa ndani ya simu yangu walipokea message iliyosomeka ifuatavyo " naomba unitumie vocha ya 5000/= nitakurudishia niko sehemu hapana duka na nahitaji sasa hivi"

Watu wengi waliibiwa kupitia kutumtumia dola.
Ninawataarifu jambo hili kwani nimegundua limemtokea na mwenzangu ofisini siku ya jumapili 21/12/08 na mimi nilituma dolla nikifikiri namsaidia kumbe naibiwa. Kwa huyu mwenzangu mbinu iliyotumika ni sawa kabisa na mbinu iliyotumika kwangu.nina wasiwasi wengi watalizwa na kijana huyu. Kijana ni smart, knowledgeable, polite looking, courageous na kimwili ni mdogo mdogo and very friendly during the discussions si rahisi kumshuku.

Kinachonisikitisha kijana yuko bright laiti angalitumia hizi sifa zake kufanya kazi rasmi naamini angekuwa mbali sana Haya ...bomu hilo kaeni macho! Tuma ujumbe huu kwa watu wowote utakaoweza ili kuwataarifu.

1 feedback :

Guest said... Thu Mar 12, 02:57:00 AM MST  

:) Ahsante sana kwa ujumbe huus rafiki na mpe Ahsante rafiki yako

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads