wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, February 12, 2009

TweetThis! DC aamuru Walimu wacharazwe viboko

UPDATE(13 Feb 2009): DC aliyeamuru walimu wachapwe viboko emefukuzwa kazi na Raisi!


Asante kwa habari bloga Rwebangira, hata na hivyo, siwezi kujibu swali ulilouliza ikiwa huu ni ulevi wa madaraka au la nadhani hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa na kama ni sheria inahitaji kupitiwa upya. Jamii ya waungwana na walioelimika huwa haifanyi mambo hivi na si rahisi hata kuthubutu kuwaza hivi.

MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali, ameacha maswali miongoni mwa walimu baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika shule tatu za msingi za kata ya Katerero na kuamuru walimu 16 kucharazwa viboko kwa kile alichodai ni utoro na uchelewaji wao.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Mnali alikiri kufanyika na kusema hao ni sehemu ya walimu wazembe waliochangia wilaya yake kuibuka na matokeo mabaya katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
“Nikamwita askari wangu nikamwambia Mwalimu Mkuu atoke, tukafunga mlango nikawaambia walimu kama watoto wanaochelewa mnawapa adhabu na mimi nawapa adhabu,” alisema Mnali kuthibitisha kucharazwa viboko vinne kila mmoja.
Alipoulizwa kama adhabu hiyo haikuwa udhalilishaji wa walimu, alikana na kusema haikutolewa mbele ya wanafunzi na kwamba yeye si mtu wa kwanza kutoa adhabu ya aina hiyo aliyoiita kuwa ndogo. Mbali na kutoa ufafanuzi huo, alisema tayari amemwandikia Mkurugenzi juu ya adhabu hiyo akiambatanisha na majina ya walimu walioadhibiwa na kusema inabidi wachukuliwe hatua zaidi kwa vitendo vyao vya uzembe na utoro shuleni.


Walimu waliocharazwa ni Generosa Lwakatare, Ernestina Anatory, Jonesta Grenos, Hawa Ayubu, Rehema Baisi, Frieda Laurian, Avitus Leonald na Asirath Ndyamukama wa Katerero.

Wengine ni Amos Kamugisha, J.K. Zale, Bruno Francis, M. Mwesiga, Pulleti Rugemalila, Winfrida Kakurwa, Editha Bigilwa, Ester Mutashaba, Ludovic Bushongole, Gosbert William, Venance Philipo na Vedasto Munabi wa Kansenene.

Walimu wengine waliochapwa ni Imelda Lwegalulira, Coretha Ernest, Devotha Bushobe, Augustina Bampenja, Josephina Ndyamukama, Julius Katemana, Videlieth Yesse, Generoza Mulokozi, Sylvester Petro, Josiah Kamuhabwa na Concessa Rweyemamu wa Kanazi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, akizungumza na Redio ya TBC Taifa jana, alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kwamba alimwagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kuwasiliana na Ofisa Elimu wa Mkoa, ambaye atawasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, na Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za kulipeleka suala hilo kwa Waziri Mkuu kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka na wakuu wa wilaya.
“Ni kweli tukio hilo limetokea … ni vyema DC na huyo Polisi wakapimwa afya kwa sababu hii si hali ya kawaida, kwani zipo taratibu za kinidhamu za kuchukua kwa watumishi,” alisema Naibu Waziri wa Elimu MWANTUMU Mahiza ambaye kitaaluma ni mwalimu.
Habari kamili, HabariLeo

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads