Film : Love in the Time of AIDS
Kanembwa refugee camp in Western Tanzania.
Noe Sebisaba.
The first Burundian refugee to come out and announce in public that he has HIV.
Noe Sebisaba.
The first Burundian refugee to come out and announce in public that he has HIV.
4 feedback :
Asante Da Subi. Nilipata muda wa kutosha kuiangalia yooote. Kwa hakika kwa kila mwenye muda na afanye hivyo. Kuna mengi ya kujifunza na kujikumbusha na kuguswa pia na maisha ya hawa wapendwa.
ASANTE SAANA KWA HIZI
Ni mpaka mtu aitizame yote ndiyo ataweza kupata ujumbe kamili na kujifunza jambo la maana ama kuwafundisha wengine. Asante kwa kuwa pamoja Mube!
Da Subi,
Asubuhi hii ya saa 11 hadi 12 hivi nimeweza kuione Film nzima ya Noe. Ina mambo mengi sana ya msingi ambayo watu tunajifunza kuhusu mambo ya ukimwi, na kikubwa kabisa haya mashirika yasiyo ya kiserikali, NGOs kufanya vitendo na sio wizi wa kutumia matatizo ya watu.
Ushauri wangu, ni kwamba watu wengi waweze kuiona film hii.Na hata itumike ktk kufundishia mashuleni, au ktk makongamano ya UKIMWI...sijui kama wengi wanajua kuna film nzuri yenye mambo ya msingi kama haya.Mfano TBC1, ITV, START TV nk wakiweka film hii ktk vipindi vyao vya kuelimisha jamii, itakua maarufu sana, na watu wengi watajifunza mengi.Sio wote wana hii access tuliyonayo ya internet.Na hata Tanzania, sio wote wanaoenda internet cafe wanaweza kutumia saa yao moja ambayo ni kuangalia film hii.
Nashukuru Da Subi kuiweka hapa film hii.Pia na ile film ya Eliza-Uwanja wa Fisi nayo ni ya msingi sana ktk mapambano dhidi ya UKIMWI.
MAKULILO Jr,
Nakubaliana na kauli yako Makulilo. Hizi ni filamu zenye mafunzo mazuri sana kwa jamii yetu. Nimezihifadhi japo mimi si mtengenezaji lakini inawezekana kabisa kuwasiliana na watengenezaji na kupata kibali cha kuzitumia kwenye vyombo vya habari kwa ajili ya elimu kwa umma. Ninachofurahi ni kuwa wapo wanaothubutu kutumia muda wao wa hadi saa nzima kutizama filamu hizi kwani zinawapa elimu ambayo wanaweza kuitumia kwa kuwahadithia wengine. Ndiko kujiongezea elimu na maarifa.