Ujumbe wa uchungu toka kwa G.S - Sheria ichukue mkondo wake.
Ni mambo kadhaa yanatendeka katika nchi hii ambayo yanawaudhi watu wengi na kusababisha kukata tamaa pamoja na kujichukulia sheria mkononi. Tunayaona kila leo yakitendeka mitaani au maeneo ya kazi, kwa wazi wazi au kificho. Jana hapa imeripotiwa habari ambayo Mheshimiwa Mbunge amewapa sentensi moja wabunge wenzie kuwa, 'tumechoka.... uvumilivu wetu utafika kikomo', mi nikaongeza kwa kusema, bora Mheshimiwa huyu kawafahamisha wenzie, muda unakwenda kwa kasi ya ajabu, nadhani wanajua kuhesabu majira na nyakati. Juzi G.S. aliandika kwa uchungu kuhusu habari ya Walimu wa Tanzania (ilitokana na kile kisa cha mtoto kuchapwa kinyama). Ni hali ambayo ameipitia binafsi kwa hivyo anajua anachokizungumza. Hali hii inafanana kabisa na hali iliyopo katika 'baadhi' ya kada mbali mbali za kazi. Alichokisema yeye kinawakilisha mawazo ya walio wengi. Ndipo nilipomwomba kutumia ujumbe wake kwa ajili ya kuwafikia wasomaji wa blogu na alikubali. Hivi ndivyo anavosema:Hapa sheria ichukue mkondo wake, ndiyo maana sheria hizi zipo sio kuzuia ualifu bali kuwafanya watu waogope kukosa kwa sababu ya mvua kadhaa. Kwa nini mzazi anamchapa mwanae? Naomba tuwaze kwa mtizamo wa Ukristo na pia kama waathirika wa kuchapwa (mf. MM Sr) Kwa wanamahesabu mvua kadhaa ~viboko alivyochapwa huyu mtoto (ingawa alikosea tu mahali pa kuchapa). Zote ni adhabu tuuu.
LAKINI NI LAZIMA TUTAFUTE SULUHISHO LA KUDUMU LA HILI TATIZO LA UNYANYASAJI WA WANAFUNZI. Sorry tatizo la kuchanganyikiwa kwa Mwl.
KWANZA TUMWANGALIE HUYU MWALIMU NA KUTAFUTA NI SHETANI GANI ALIYEMFIKISHA HAPA NA PIA HUYU SHETANI AMETUMIA NYANJA GANI KUMFANYA HUYU MWALIMU ACHANGANYIKIWE. LAKINI PAMOJA NA KWAMBA HUYU MWANAFUNZI KUCHAPWA NI MATOKEO TU, HUYU MWANAFUNZI AMECHANGIA VIPI KWA KUCHAPWA KWAKE?
Mwalimu Mwalimu, mwalimu wa tz.
Du!
Mwalimu wa tz tena kule kijiji,
“Mtendakazi anahitaji kupata ujira wake”
1) Anaanza kazi kwa madeni, atalipwa sallary baada ya mwaka mmoja na zaidi.
2) Atakuwa anaishi nyumba ya kuombewa pale kijijini kwani hana pesa ya kulipa pango.
3) Hivi atakuwa anakula nini, analala wapi, anavaa nini?
4) Ila hiyo nyumba aliyoombewa kuishi kwa mkopo hadi apate mshahara ili alipe pango ni nyumba au tembe, pagale, full suit, mbavu za mmbwa?
5) Hapa kijiji hana source nyingine ya income, yeye na chaki, chaki na yeye, Scheme of work, lesson plan, lesson notes, teaching aids n.k. kwa madarasa yote saba mwl mmoja au wawili.
6) Akiwa anajiandaa ku-settle ghafla vile viatu vyake vya college vinaanza kuchakaa kwa kukosa kiwi, hivyo vidole vinaanza kutafuta uhuru, nadhani kitaanza kidole kikubwa cha mguu, ataenda kwa fundi viatu atambembeleza weee amshikie shikie tu atamlipa mwezi ujao kwani alidanganywa hivyo wa wana si hasa kuwa ni lazima walipwe pesa ya kujikimu na malimbikizo ya mshahara wao mwezi ujao. Wapi?
7) Mtaa mzima wanafahamu mwalimu analalia kirago, hata wale watoto anaowafundisha wanajua hilo, hamna hata kigoda ndani, hapo kuna adabu?
8) Du! nimemkumbuka mwalimu wangu mmoja, mvua ikinyesha vidole vilishatafuta uhuru na mvua ikinyesha basi taabu tupu, anapotembea darasani akikagua kazi za wnfz, kiatu kinatema maji maji tu. Maskini mwl!!!! Afanyeje? Si mlimtuma bwana akajenge taifa la kesho kama mnavyosema?
9) Ghafla baada ya miaka kadhaa, Wizara imeota ameanza kulipa mshahara, ila pesa ya kujikimu(kumwezesha kuanza maisha) bado. Si wanadhani hajaanza maisha? Hayo anayoishi miasha nayo? Wenye maisha njoo bongo-Osyterbay huko na Ma-STK, STH+ full kiyoyozi, watoto wao wanasoma hizo shule zinazochapa hizo? Uwachape hujipendi? Wengine wako nchi za watu wanapata elimu, au shule zile za kirengesa n.k. Tuache hizo nanii, tunazaliwa sawa, tunakufa sawa ila hapa katikati madaraja kibao, makabaila, mabepari, magabachori, wakoloni, matawi ya juu, na walalahoi n.k. Hawa wote walifundishwa shule zile zile za mchonga al- maarufu mwalimu. Tuendelea kumwangalia mwl wetu anaeambiwa sheria ichukuwe mkondo wake.
10) Anaanza kupiga mahesabu kuufuata mshahara, baada ya kutembea Km kadhaa kwa mguu anatakiwa alipe nauli 1/3 ya sallary, aondoe pesa ya guest n.k. Anabakiwa na pesa za madafu ngapi kwenye hiyo sallary ya $112?
Akirudi kijiji kila mwenye kibanda(kwani kijiji kuna maduka?)anamdai. Unaona mtihani mkubwa hapo, aanze kumgawia nani? staff wenzake, mwenye pagale, wauza vibanda, anunue godoro, au sufuria, du! NAOMBA WATAALAM WA OFISI YA RAIS MIPANGO WAMWAMBIE ABUDGET VIPI.
11) Kwa mantiki hiyo hatakaa amalize madeni, kwani hiyo pesa ya mshahara hata matumizi ya mwezi tu, haitoshi.
12) Kama Mwl huyu ana huruma kweli atakutana na mambo ya ajabu huko shule wapo watoto yatima na masikini hawana kalamu, daftari, anakuja shule tangu alipokula chakula cha shule(kama kipo)jana yake, hakijaingia kitu kingine mdomoni, huruma ya mwalimu anaweza akaanza kugawa umasikini wake kuanza kutoa msaada (kama upo). Au huelewi kuwa hata angefundisha vipi hayo mahitaji ya msingi lazima yawe yametimizwa kwanza. Unamkumbuka Erickson?
13) Sijaanza kukumwambia habari ya workload yake, we unadhani kuna mwanadamu anapenda shida? Nani atakubali kwenda huko? Nani? Nakuuliza wewe utaenda ukabidhiwe shule yenye madarasa 7 na mwl 1 au 2. Utaenda? Anaanza na wale wa darasa la kwanza, inabidi ajifunze kilugha kwanza, kwani wanajua kiswahili hawa? Kama kwao alikuwa last born, na hajajifunza kumlea mdogo wako ataanza kujifunza hapa, mara mwingine kajisaidia haja great & small na mwingine zote, mwingine makmasi, mwingine, kamfinya mwenzake, ili mradi vurugu tupu. Akitoka hapo aende darasa la 2,3,4,5,6,7,8 n.k. Mi sijui atafundisha somo gani hapo, anyway hata akibuni mtaala wake mwenyewe ayachanganye yote its ok. Kwani afuate mtaala wa tz yuko tz yeye?
14) Ghafla kaja mkuu wa Wilaya baada ya kulalamikiwa na wazazi, njiani kachuma fimbo kadhaa za kuwageuzia kibao hao jamaa wanaoichezea serikali(Inatisha!!!!). Ghafla mwl anapewa order lala chini, nimesema lala chini, kwani yeye si yuko juu ya sheria Bwana. Afande linda usalama wa raia hapa, kung’uta kadhaa hapo. Du! Teacher teacher pole sana pole sana. Wala hakuna atakaekusupport kwamba huyu Mkuu wa Wilaya achukuliwe sheria. Lakini ole wako baada ya frustration zote hizo umchape mwf? Wataamka na makelele- sheria ichukue mkondo wake, sheria ichukue mkondo wake. Du! Haswa ikiwa uliyemchapa ni binti mara watetezi wa haki za wanawake, watoto, wnfz watajitokeza wamepata kazi hapo, waandisha wa habari nao wamepata yakuandika. Tuandike tufanye kazi za utetezi jamani, ila tutafute mizizi ya mchongoma huu ili tuung’oe, watoto waliobaki shuleni hawataonewa, tukishang’oa mizizi ya hili lijitu linalofrustrate mwl wetu.
15) Wale waalimu ambao hawajafikia level ya mwenzetu, nawapa hongera kwa uvumilivu, ila tuungane wote kumng’oa huyu anaetufrustrate. Yale tuliyofundishwa chuoni Saikolojia ya makuzi, malezi n.k, ushauri nasaa n.k. tujaribu kuyakumbuka ingawa hawataki tuyakumbuke. Najua iko siku atatoka mmoja wa hao tuliowapenga makamasi na kuzoa haja zao great kule darasani akatukumbuka. “Yote haya yanamwisho” by Rashid in Kuli, au unataka niwaambie waalimu waendelee na mgomo? Hata nikiwaambia hawatasikia acha kunielewa, si wanaogopa mkuu wa wilaya kuwachapa kiboko.
16) Unawakumbuka wale uliosoma nao O-Level na wakaenda ualimu kijiji, wako je sasa hivi? Wengine wakikuona wanakimbia, kwani wao watanzania? Si unaweza ukaita mgambo wa jiji kukamata hawa wazururaji kwa walivyovaa? Si unaweza kuwapeleka kwa mkuu wa wilaya? We unadhani mwl anapochapa anapenda kuchapa yeye? We unadhani anapenda kuchapwa yeye? Kamuulize.
Yanaanza kutoka machozi sitaki na wala siwezi kuendelea.
MAFRASTRATION HAYA YOTE, SI NAFUU AKAJISALIMISHE MWENYEWE MAGEREZA HATA BILA KUPITA MAHAKAMANI? KULE CHAKULA KIPO, HATA KAMA KWA MSOTO, LAKINI KIPO.. KULIKO HUKU KIJIJI, HANA NDUGU, HANA MJOMBA.
Nilikuwa nafikiri tu, ila tusianze kuzungunza baada ya tatizo kutokea, kama wasomi tuone tatizo kabla halijawa tatizo, tulidhoofishe kama sio kuliangamiza mizizi yake. Huyu anaweza kuchukuliwa sheria akafukuzwa kazi kwa kuwa amesha-disqualify kuwa mlezi, kisha akafungwa, lakini hawa walimu wengine jamii inaowalelea/ kuwaandaa ili wachanganyikiwe watafanya nini? Yumkini mimi na wewe tusipochukua hatua leo wanaweza kuleta madhara makubwa zaidi kesho. Shikamoo mwl.
SOLIDARITY FOREVER
3 feedback :
Huu ni ukweli mtupu. Inasikitisha!
Pole 'Solidarity Forever': umetia pilipili kali lakini pengine mengi ni ya kweli katika "bongoland". Sehemu yetu ya Iringa sijui kama mambo haya yamo, bila kukataa magumu mengi kimaisha kwa Walimu! Lakini walimu hawana haki ya kurudisha kisasi kwa watoto au kuwamwagilia 'frustrations' zao! Kweli watoto wana haki zao hata kwenye 'bongoland'.
Yule aliyenynyaswa kwa kupigwa ovyo lakini ni kwenye shule ya secondary, tena hapo MJINI NA MWALIMU wa muda mrefu.
Anonymous wa Wed Jul 29, 11:05:00 AM Pole sana kwa kuguswa na tatizo la Mwnfz huyu. Pole sana.
Ni kweli hawana haki ya kurudisha kisasi kwa wnfnz, ni kweli kabisa. Huyu ni wa sec, sawa kabisa. Kumbuka wapo waliopoteza maisha, waliopewa ulemavu, walionyimwa haki ya kusoma na waalimu n.k.
Kuchangia kwangu, sikusema amefanya vizuri au asichukuliwe hatua. Bali nilijaribu kufikiria kama binadamu mwenye utashi, na muhathirika wa manyanyaso ya jamii na serikali kwa waalimu. Dawa ya kuzuia haya manyanyaso ni kufikiria zaidi ya kumpeleka huyu mwl mmoja wa Iringa mahakamani tu. Tutafiti na kuyajua yaliyomsukuma huyu mwl afanye hayo, twende vijijini tuone hayo ambayo hujui kama yapo Iringa, kwani nina imani yapo kabisa. Ebu fikiri nami, kama huyu mwl mzoefu kama ulivyosema tena wa mjini amefanya haya, huko vijijini ambako mwl ndiye, hakimu, daktari, mshauri, ndiye msomi, yule aliyesoma ualimu kwa miezi kadhaa na hana uzoefu atafanya nini? Twende tukachunguze, utaona mambo ya ajabu mno mno. Sehemu ya pili ya sarafu, tuchungunze hawa watoto, wanawasaidia je hawa waalimu kutimiza lengo lao la malezi. Siku hizi ninaogopa binafsi hata kumwonya mwnfz wa kike, anaweza kukuzushia kashfa kuwa ulikuwa unamtaka kimapenzi. Wapo wanafunzi ambao hawana malezi toka kwa wazazi na wanawatia waalimu majaribuni, haya yamenikuta.
Naendelea kuwaza tuu