wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, July 23, 2009

TweetThis! Tunaomba mchango wa mawazo kuhusiana adhabu hii

Sikatai kwa asilimia 100 kuchapa mtoto kiboko cha maonyo, lakini inapofikia hatua kama hii, kweli kuonya kwa kiboko ni fundisho ama ni ukatili?
Huyu ni mtoto wa kike, amechapwa na mwalimu wake wa kiume, ni katika Sekondari moja huko Iringa, imetokea jana July 22, 2009, mtoto akaogopa kwenda polisi au hospitali kwa kuhofia kwa mwalimu atamwadhibu zaidi. Aliyenitumia picha hii anasema kisa cha kuchapwa hivi ni hasira iliyojificha kwa mwalimu huyo kwa kushindwa kutimiza azma yake nyingine toka kwa binti huyu.
Nimetumiwa picha hii toka Iringa, aliyenitumia hajajua jambo muafaka la kufanya, naomba kuweka kwenu ili watu wajadili na kutoa mapendekezo kipi kifanyike kuhusiana na hali hii.
Mapendekezo yenu nitayafikisha kwa aliyenitumia picha hii kwa hatua zaidi atakazoweza kuchukula kulingana na maoni yenu.

Sehemu ya ujumbe ulioambatanishwa na picha inasomeka kwa uchungu hivi:

Tupo mwaka 2009 na haya ni bado kawaida kwenye shule nyingi! Tunaimba Tanzania x2 Nchi ya Amani! Vita hii itakwisha lini? Kweli nimechukia sana kwani kamsichana huyu ni mwema na mpole!

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads