wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, January 22, 2009

TweetThis! Zawadi Bibi Sarah Obama alizompa mjukuu wake

Bi Sarah Obama aliifunga safari yake kuelekea huko Marekani kuhudhuria na kushuhudia maapisho ya mjukuu wake ambaye ni Raisi wa 44 wa Marekani, bw. Barack Obama. Kama ilivyo jadi, bi Sarah hakujiandaa kwenda kumwona mjukuu wakali mikono mitupu bali alijifunga kisawasawa kama ilivyo ada ya mila na desturi kwa kubeba zawadi murua.

Bi Sara alifungasha kigoda cha miguu mitatu, mkuki na ngao pamoja na mshipi kwa ajili ya kumpatia huyo mpendwa mjukuu wake. Lengo la Bi Sarah, ingawaje zuri kama ilivyo kwa watoa zawadi za dhati, kwa bahati mbaya lilikumbwa na dosari pale alipofahamishwa kwamba kutokana na sababu za kiusalama asingeweza kubeba mkuki huo.
Mama Sarah Obama"Nilitaka nimpe na mkuki pia, lakini nimetaarifiwa kuwa kutokana na sababu za kiusalama, sitaruhusiwa kupanda ndege na kifaa hiki". - Bi Sarah alilitaarifu gazeti la The Standard.
Wakati bi Sarah anaondoka kijinini Nyang'oma, Kogelo kuelekea Nairobi, kulikuweko na kundi kubwa la waandishi wa habari wa ndani na nje waliotaka kuchota habari na kurekodi mambo ya kihistoria. Bi Sarah alisema, 'siku niliyoisubiri kwa hamu hatimaye imewadia.... siwezi kuificha furaha niliyonayo,' alisema na kuongeza, 'Ninakuwa balozi wa Kenya katika tukio hili'.Mama Sarah Obama arrives at Kisumu Airport on SundayKama ilivyo kawaida kwa jamii zetu kusafiri na ndugu ama jamaa kwa ajili ya safari ya sherehe yoyote, Bi Sarah naye aliambatana na mwanae na mkwewe, yaani Said Obama na Beatrice, vile vile alikuwepo msemaji wa kijiji cha Kogelo bwana Nicholas Rajula na Mkewe Nelly, pia Mwenyekiti wa shule ya upili/sekondari ya Senator Obama Kogelo na Mkuu wa shule hiyo, Lynn Yaya bila kumsahau Ida ambaye ni dada wa mke wa Raila Odinga ambaye ni Waziri Mkuu wa Kenya. Ama kweli timu ilisheheni ujumbe mzito.

Akizungumza kwa lugha ya Luo kabla ya kuondoka Kenya, bi Sarah alisema, "Tunakwenda kumsimika ili auhudumie ulimwengu" huku akicheka, aliendelea kusema, '...atakaponiona atakuwa mwenye furaha tele kwa vile atakuwa ameiona damu yake'... aliongeza kuwa, "...ina hakika Barack atafurahi kuniona. Kuwepo kwangu kutakuwa na maana kubwa sana kwake".
Stuli miguu mitatu
(Kom Nyaluo)
Flywhisk
(Orengo)
Mkuki na Ngao
(Tong)
Luo Traditional Three-Legged StoolFlywhiskA group of Luo warriors - in full warrior dress with long spears and shields.
“Rajula tried to carry a spear to give Barack when he won the Senate seat but he was blocked at the airport,” she recalled. After the inauguration, Mama Sarah said it would now be upon Obama to work hard and ensure he helped those suffering across the world. In Kogelo, among those who bid her farewell included senior official of Maendeleo Ya Wanawake Organization in Siaya district, Mrs Patricia Apoli, and members of the Kogelo cultural committee who were putting final touches to a cultural festival that is set to start on January 16 at Kogelo Primary School to celebrate the installation of Obama as President of the United States.
Picha za zawadi zimehifadhiwa na: Political articles

2 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads