wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, January 23, 2009

TweetThis! MTanzania yu mahututi nchini Ethiopia kwa madawa ya kulevya

Tatizo la madawa ya kulevya likiendelea kuiumiza jamii yetu kwa kuondoa uhai wa vijana wengi ambao ni nguvu kazi ya Taifa, habari kutoka mjini Addis Ababa nchini Ethiopia zinathibitisha kuwa raia mmoja wa Tanzania amelazwa katika hospitali ya Hayat akiwa mahututi kutokana na kupoteza fahamu akiwa kwenye ndege.

Abiria huyo aliyekuwa akisafiri kutoka Tanzania kuelekea China kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia alikutwa na madawa ya kulevya tumboni mwake.

Dk. Behailu Haile ambaye ni Mkurugenzi wa hospitali alikolazwa MTanzania huyo, ameliambia shirika moja la habari la nchi hiyo kuwa MTanzania huyo alipofanyiwa vipimo vya uchunguzi tumboni alikutwa na tembe kadhaa zenye uzito wa gramu 15 kila kimoja huku kiasi kadhaa cha viroba hivyo kikiwa tayari kilishapasuka tumboni mwa mtu huyo. Hadi sasa tembe zipatazo 109 zimeshatolewa tumboni mwa MTanzania huyo. Daktari huyo alipoulizwa juu ya hali ya mgojwa alishindwa kuthibitisha ikiwa mtu huyo ambaye ameshapoteza fahamu kwa muda wa zaidi ya siku mbili sasa ataweza kuwa hai.

Mkuu wa kitengo cha polisi kinachoshughulika na uzuiaji wa makosa mbalimbali nchini Ethiopia ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa kitengo hicho bwana Asamnew Harka amesema kuwa suala hilo limeshafikishwa katika ofisi yake na kuwa wanalishughulikia hasa zaidi katika kutaka kufahamu aina ya madawa yaliyotumiwa na maelezo ya kina ya aliyekuwa ameyabeba.

Msaidizi wa mkuu wa kigengo hicho, kamanda Tsegaye Woldehiwot naye alipoulizwa alisemakuwa suala hilo ni la kipekee kwani kiasi cha tembe kilichopatikana kutoka tumboni mwa mtu huyo ni kikubwa mno. Alisema kitengo chake kimejizatiti kupambana na njia yoyote ya usafirishaji wa madawa ya kulevya na kuwasihi raia kuwa upande wa polisi katika kushughulikia masuala hayo.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads