Anti-Virus
Ikiwa una kompyuta yenye Windows ni vyema kuwa na ulinzi kiasi wa nyaraka zako kwa kuweka kinga kiasi fulani ili kuepa usumbufu wa rejareja. Nimewahi kutumia anti virus mbalimbali za bure kwenye IBM laptop yangu. Kwa bahati nzuri AVG anti virus toleo la bure ilinilinda. Kwa bahati mbaya, nilipokosa shughuli ya maana, nilianza udadisi binti peruperu wa mtandaoni. Yaani nilipokutana na software za bure mi likawa langu moja tu, chomeka kwenye laptop uone inavyokuwa. Nilisambaa kwenye tovuti nisizozijua mwanzo wake wala mwisho wake. Breki niliitia bila kupenda siku moja nimepatwa na 'blue screen of death'. Hapo ndipo adabu illiponikaa. Nilisumbuka na hadi nilipogundua kilichonisibu kuwa ni 'trojan' alijetoka kwenye mojawapo ya software za bure, nawashukuru walioanzisha AntiRootKit iliyong'oa 'trojan' ile.
Ni juzi tu (Mei 26) nimesoma maoni ya wadau bloguni kwa kaka Mjengwa na Michuzi kuwa haishauriwi kuwa na zaidi ya anti virus moja kwenye kompyuta moja ndipo nilipong'mua kuwa ni kwa urahisi gani yule 'trojan' aliyenisababishia 'blue screen of death' aliweza kuivaa laptop yangu. Itakuwa tu wakati hawa anti virus watatu wanatuhumiana na kuhisiana kuwa mwenziwe ndiye mwizi (fahali wawili hawakai zizi moja seuze mimi niliwaweka watatu), kumbe ndo papo hapo 'trojan' aliwapita na kuilamba laptop yangu.Msomaji wangu, wacha nikupe orodha ya anti-virus za bure, chagua moja tu. Ukitaka ulinzi zaidi, weka na spyware na firewall (ikiwa Windows Defender Firewall haipo katika kompyuta yako, inapatikana bure katika tovuti ya Microsoft).

Best Free Anti Virus you can choose from:
Orodha mchanganyiko ya Anti Virus, Anti Spyware na Firewall ipo ITSecurity - 103 Best Free Secutiry Utilities.
Kwa msaada zaidi wa kuamua aina gani ya Pro Anti Virus ununue, tafadhali tizama mlinganisho uliandikwa kwenye 2008 Anti-Virus Software Top Review
0 feedback :