wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, October 11, 2009

TweetThis! Chanjo ya UKIMWI yagundulika Tanzania (ni kweli?)

Habari hii nimeotoa kama ilivyoripotiwa na Peter Mwenda na kuchapishwa katika gazeti tando la Majira.co.tz

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Kisali Pallangyo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu matokeo mazuri ya utafiti wa tiba ya ugonjwa unaodhoofisha kinga ya mwili kupambana na maradhi (UKIMWI) waliofanya kwa kipindi cha miaka 19 ambao umeonesha mafanikio makubwa. Kushoto ni mmoja wa watafiti ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa David Ngassapa. Utafiti huo umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 5. (Picha na Charles Lucas)
CHUO Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS) kimesema majaribio ya utafiti wa chanjo ya kutengeneza kichocheo cha kinga dhidi ya maabukizi ya virusi (VVU) umeonesha mafanikio makubwa.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Kisali Pallangyo akizungumza Dar es Salaam jana alisema utafiti ulioanza mwaka 2007 na unaondelea katika chuo hicho umepata mafanikio ambayo yamesaidia kupatikana kwa chanjo ya kukinga maambukizi ya virusi vya UKIMWI. "Majibu ya utafiti wa chanjo ya kukinga maambukizi ya VVU katika Chuo cha MUHAS ni mazuri sana, walioshiriki wote ambao tumewachanja asilimia 100 miili yao imetengeneza kinga ya UKIMWI," alisema Profesa Pallangyo. Alisema baada ya mafanikio hayo MUHAS inatarajia kuwasilisha ripoti hiyo wiki ijayo kwenye hoteli ya Ngurdoto, Arusha na baadaye kwenye mkutano wa chanjo ya UKIMWI utakaofanyika Ufaransa Oktoba 19. Profesa Pallangyo alisema matokeo ya majaribio hayo ambayo yameonesha kutengeneza vichocheo vya kinga dhidi VVU, yanafanana na majaribio ya awamu ya kwanza nchini Swideni,nchi ambayo pia ilitoa fedha za kufanya utafiti kupitia Shirika lao la Maendeleo la Kimataifa (SIDA) ambalo lilitoa fedha za kununulia vifaa na kufanya utafiti.

Mkurugenzi wa Mafunzo wa MUHAS, Dkt. Muhammad Bakari alisema majaribio ya chanjo ya VVU kwa binadamu yalifanywa kwa askari polisi baada kutimiza masharti ya kutokuwa na maambukizi ya VVU ambao wamefanyiwa majaribio ya chanjo ya kuangalia usalama na uwezo wa kutengeneza kinga. Dkt. Bakari alisema japokuwa chanjo hiyo imeonesha mafanikio katika kuzuia maambukizi ya VVU lakini hakuna uhakika kwamba inaweza kuua virusi vya UKIMWI kwa wagonjwa ambao tayari wanaugua ugonjwa huo. Alisema chanjo hiyo inawezesha mwili kutengeneza vichocheo vya kinga ambavyo huenda vikatoa kinga dhidi ya maambukizi ya VVU na kuimarisha zaidi uwezo wa kitaalamu katika kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya VVU nchini Tanzania. Dkt. Bakari alisema utafiti huo ambao umefanyiwa majaribio kwa washiriki ambao ni miongoni mwa askari Polisi polisi 60 wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao walikubali kwa utashi na ridhaa yao na katika majaribio hayo hapakuwa na madhara yaliyotokea baada ya kupatiwa chanjo hiyo. Alisema majaribio hayo yalianza kufanyiwa polisi hao baada ya kutimiza vigezo vya kutokuwa na maabukizi ya UKIMWI,afya njema na wenye uwezekano mdogo wa kupata VVU ambao kutokana na ujasiri wao wanastahili kupewa heshima ya kishujaa kama wale wanaokwenda mstari wa mbele vitani.

Katika warsha hiyo, Mratibu wa Maabara wa MUHAS, Profesa Eligius Lyamuya alisema washiriki 24 kati ya 52 walipatiwa chanjo hiyo walifanikiwa kutengeneza vichocheo vya kinga dhidi ya VVU, baada ya kupata chanjo 3 za DNA. Alisema washiriki 35 kati ya 48 nao walitengeneza vichocheo baada ya kupata chanjo ya kupiga jeki na katika chanjo ya tatu washiriki 23 kati ya 59 wametengeneza vichocheo na wengine 34 kati ya 50 walipata chanjo hiyo walipata mafanikio kwa asilimia 100. Profesa Lyamuya alisema pamoja ya mafanikio hayo chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya kuongeza maabara, wafanyakazi wa maabara na kuongeza vifaa vya maabara.

Naye mtaalam wa kinga na magonjwa yanayosababishwa na virusi, Profesa Fred Mhalu na alisema chanjo hiyo isiwe kichocheo cha kufanya ngono bila kufuata ushauri wa kitaalamu wa kuacha kujamiiana na kuchelewesha ngono kwa vijana hadi umri wa kuoana au kuishi pamoja, uaminifu kwa wenye ndoa ambao wamepima na matumizi ya mipira ya kiume au ya kike ambayo ikitumiwa vizuri hukinga kwa asilimia 90. Alisema Tanzania yenye watu watu milioni 40, kati yao, watu milioni 1.4 wameambukizwa virusi vya UKIMWI. Kati yao 760,000 ni wanawake na watoto wanaoishi na virusi ni 140,000. Profesa Mhalu alisema kutoka utafiti huo uanze kufanyika MUHAS umetumia gharama za majaribio ya kutafuta chanjo ya VVU ya Sh.bilioni tano ambazo zimetumika ajili ya kununua vifaa vya kupima vinasaba na kwa sasa imeanzisha programu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mafundi wa maabara.

4 feedback :

Anonymous said... Sun Oct 11, 03:10:00 PM MST  

Dada Subi ebu tuhabarishe kidogo,kwani hii habari ni nzuri lakini imeandikwa kisanii fulani hivi.Habari kubwa kama hii,matokeo makubwa kama haya, hayatakiwi yaandikwe kama ripoti ya kisiasa.

Tungependa tujirizishe kwa vitu muhimu kama,
Huo utafiti ulifanyika vipi? Ili na jamii ya wanasayansi wakubali.Sio wasomaji wote ni mbumbumbu.

(1)Matokeo ya control na experiment groups,si kutupa ya experiment group results peke yake.Kama hakuna control wamewezaje kuconclude au wataendelea na phase II,kama ndivyo,ntakubali hapo.

(2)Je? percentage protective power ni ngapi, si kutupa idadi tu ya waliotengeneza kinga.How do they define protection? forming antibodies or effective power to prevent multiplication and diseemination of HIV virus? killing power of the antibodies?????

(3)Je wanadifine vipi kutengeneza kinga.je kutengeneza kinga ni sawasawa na kuwa protective, kama sawa ni kwa percentage ngapi. (The ability to form antibodies doesnot directly translate into 100% protection,doenst confer 100% protection).Je vipi suala la infective dose??

(4)Je wamecontrol vipi uhusiano wa kiasi cha antibodies kilichotengenezwa na protective power,nikimanisha sio wote waliweza kutengeneza enough antibodies to confer maximum immunity.ni ratio ya wangapi waliotengeneza antibodies za kutosha kuprovide protective power against HIV kati ya idadi kubwa ya waliotengeneza antibodies, je ? hao watawajumlisha kwenye idadi ya walio na kinga au watawaweka kwenye idadi ya wasio na kinga.(To have antibodies doent translate to having enough and the required amount of antibodies/immunity.

(5) For how long does the power of the antibodies formed last.one month,two months,three years. na kusema hapakuwa na madhara yeyote kwa waliochanjwa ni uhongo.Bora wangesema hapakuwa na reported cases of severe side effects.

Labda tusubiri ripoti nzima, ila hii ya sasa haijitoshelezi kabisa.Hii ripoti inanikumbusha ripoti ya utafiti wa uhusiano wa circumcision and HIV, ambapo waliconclude circumcison confer >30% protection against HIV.Huo utafiti ukiuchunguza, una makosa kibao ya kiutafiti kiasi kwamba nachelea kusema "the study was frauded" they grossly failed to account for other factors which could have enterfered the effects of the independent variable they were testing (circumcision) or could have added more strenght to the power of circumcion.

Yaani ningeburudika sana kama ningekuta maelezo ya kwa namna gani waliweza kucontrol for confounding factors and effects modifiers, kwani bila ya kufanya hivyo, tunakuwa hatuna huakika na conclussion ya mwisho ya utafiti.Je hawa watu wamekingwa dhidi ya HIV hata kama vijidudu vikiingia, na kwa asilimia ngapi?. Je observation time inatosha kuconclude.

Anonymous said... Sun Oct 11, 07:26:00 PM MST  

Hello dada Subi.

Kwa kweli kama hii habari ni ukweli this will be the best news the world has heard in a long time of trial of vaccines and limited success. I cant wait to read the published paper please keep us posted if it comes out on a scientific journal.

Mdau far from home
Huntsville, Al. U.S.

Anonymous said... Mon Oct 12, 10:49:00 AM MST  

Kwa kweli kichwa cha habari kinamislead kabisa,labda kama hayo matokeo ni matokeo ya mwisho katika final phase of their trial, kitu ambacho sitegemei kutokana na report.Wangesema. UTAFITI WA CHANJO YA UKIMWI WAONYESHA DARIRI/MATOKEO MAZURI"HIV trial revealed promising results".Kazi kwelikweli, sijui ni makosa ya muandishi au ni watoa report wenyewe walitaka kuvuta attention.

Kama ndiyo ilikuwa report yao, watakuwa wamewamislead watu vibaya sana.Kuna promising results kibao zilipatikana na zinapatikana kwenye trials nyingi lakini baadaye kwenye final phase inakuja kugundulika kwamba the anticipated consequences exceeds the potential benefits.na utafiti unakuwa aborted. Tuwe makini kwenye kuripoti hizi taarifa muhimu za kisayansi. Ebu tusubiri final paper kama alivyosema mjumbe mwingine hapo juu

Subi Nukta said... Mon Oct 12, 11:25:00 AM MST  

Ninaafiki hoja zenu, ndiyo maana hata mimi kwenye kichwa cha hababari hapo nimewekwa kwenye mabano (ni kweli?) maana maswali ni mengi kuliko majibu.
Habari hii nimeipata kwenye gazeti lakini sijafanikiwa kupata haswa taarifa ya utafiti wenyewe, sifahamu ni lini wataiweka hewani, naisubiri kwa hamu na kama waliipitisha kwenye vikao vyao bila ya kupata 'constructive criticism and enough questioning', huu utafiti "watanyonywa macho" kwenye international health, research and scientific bodies kabla ya kupewa kisogo halafu tuanze kulalamika dharau au tunabaguliwa.

Sijui, wacha nisubiri, nikiipata ripoti nitaiweka hapa, mkiona kimya mjue bado wamebana, si unajua ripoti za kwetu zinavyofichwa kwenye briefcase na makabati halafu zikitolewa zinawekwa tayari zimeshapitwa na wakati zinabakia kuwa 'zilipendwa' na kukamata vumbi kwenye mafaili tu kabla ya kuingia mtaani kufungia vitumbua na kuanikia pweza.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads