wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, September 11, 2009

TweetThis! Wakati wa kula raha, kuosha vyombo je?...

Baadhi ya wanaume kwa kweli akili zao huwa zimejaa ulanzi linapofikia suala la kukubali matunzo na malezi ya watoto wao wanaowazaa wenyewe wa, "nje" ni "bahati mbaya ya kutokutarajiwa". Kumbe wanapokwenda kumtongoza huyo mwanamke wanatarajia baada ya kuparamiana kusikae kutokee kiumbe humo? Ndoto za juha. Ikiwa ni rahisi hivyo basi wakikemee na mapema hicho kimiminika kinachowatoka kwenda kuungana na cha wanaoparamiana nao katika kutunga mtoto, vinginevyo watulize mishawasha yao ambayo mingi huishia kusambaza VVU na gono tu.

Eti huyo mwanamke si angekataa? Na wewe kilichokukataza kukataa kipi hasa? Yeye aweze kukataa na wewe ushindwe una lipi? Hata angekataa, ungekubali? E babu, ukishindwa kutuliza mpira wako mapajani vile vile ujue na mwenzio si malaika aweze kutuliza manyanga yake kiunoni.

Ikiwa mlitenda pamoja na matokeo ya kutenda huko myapokee kwa pamoja. Ikiwa huna imani kama ni mwanao, nenda kapime uhakikishiwe, umzodoe huyo anayekuchongea, lakini usibishe na kuruka kimanga kama juha. Hizi si zama za kuuziwa mbuzi kwenye gunia na kukubali hovyo hovyo tu.

Nimefurahishwa sana matokeo ya kesi hii ambapo aliyekuwa mheshimiwa saaaana mkuu wa Jeshi la Polisi wakati fulani emeamriwa kulipa matunzo kwa mwanae
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam imemuamuru aliyekuwa Mkuu wa Polisi (IGP), Omar Mahita atoe sh 100,000 kila mwezi kuanzia leo kwa ajili ya kumtunza mtoto aliyemtelekeza. Mahakama hiyo pia imemuamuru Mahita alipe malimbikizo ya sh 100,000 kila mwezi tangu alipomtelekeza mtoto huyo, Juma Omar Mahita, mwaka 2003. Habari kamili zinapatikana katika HabariLeo.co.tz na DarLeo.co.tz
Yaani raha kula, ikifika zamu ya kuosha vyombo haikuhusu, baadaye chombo kikiwa safi watang'ang'ania ni chako. ebo, uwage na soni!

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads