wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, August 03, 2009

TweetThis! Namba za dharura za Polisi Tanzania dhidi ya uhalifu

Leo katika tembelea yangu mtandaoni nimekutana na habari kwenye kundi pepe fulani ambayo mmojawapo wa wanachama wake aliituma kama TAHADHARI. Kama ilivyo ada ya penye wengi pana mengi, baadhi ya wanachama wa kundi hilo walidai uthibitisho wa namba hizo na kuonesha wasiwasi ama kudhani ni utani na hivyo kudharau onyo la ujumbe huo. Hata na hivyo, hala hala ni mti na macho, ama lisemwalo lipo, ikiwa halipo lisubiri laja, ujumbe ulitumwatarehe Jul 27, 2:35 pm na mnano tarehe ya Julai 31, iliripotiwa uhalifu na wizi wa fedha katika benki ya NMB Temeke, Dar es Salaam.
Ujumbe huu ungezingatiwa ikiwa tungekuwa na mawasiliano madhubuti ya intaneti na vyombo vingine vya habari, huenda ingesaidia kwa namna moja au nyingine. Hata na hivyo, namba zilizopo hapo zinaweza kuhifadhiwa kwa matumizi ya siku zijazo. Ujumbe unasema:
Tafadhali wajulishe wote wanaohusika kwamba kuna kundi kubwa la majambazi wenye silaha kali, ambao wameingia Jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wahalifu hao ni pamoja na (jina la nchi jirani) ambao wana tabia ya kupora fedha katika taasisi kubwa kama, mabenki, kampuni za mafuta na sehemu zenye biashara kubwa n.k . Aidha watu hawa wana mbinu ya kula njama na watumishi wasiokuwa waaminifu. Ni muhimu mkafuatilia mienendo mbalimbali katika benki zenu na sehemu zilizotajwa hapo juu pamoja na kuimarisha usalama julisheni kwa message kupitia namba 0783-034224 au kwa simu ya mdomo 0754-034224, 0787-034224 , zote ni namba za Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam. Namba zingine za simu ni 0754-276217, 0776-880000 namba hizi ni za mkuu wa Upelelezi Kanda maalum.

Lengo la maelezo si vitisho kwenu bali ni tahadhari muhimu , inayofaa kuzingatiwa.

S. H. Kova - SACP
KAMANDA WA KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Imetolewa katika kundi pepe la ex-Bunge

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads