Funny: Lazima tujue humu huwa wanaweka nini humu...
Nyani nao hawana simile, kila kitu wanapenda wachokonoe hadi wajue kunani. Walipatia kweli kweli kwa watalii hawa. Ni kama vile kila mmoja alikuwa anasubiria chake cha kumtoa, kila mmoja anasubiri kwa hamu. Cheki bobu mmoja kapata kofia ya kutesea mtaani, katoka chicha ile mbaya, lazima watamkoma! Nyani wadadisi...
Habari kamili inapatikana: http://www.knowsley.com/s_park/news.asp?rid=76
Habari kamili inapatikana: http://www.knowsley.com/s_park/news.asp?rid=76
3 feedback :
OMG.NIMECHEKA MPAKA!HAWA NYANI SIJUI NI WAFUASI WA MATONYA? LAKINI HAPANA,NAZANI NI WAJASILIAMALI WADOGO... WAMACHINGA? WANATAKA KUINGIA MITAANI NA BIASHARA YA MITUMBA,HUYO MWENYE KOFIA NDIO BITOZI,MBONA MTAANI WATAMKOMA HAHAHAHAAA UJANJA KUWAHI.
Passion4Fashions.Tz, mie pia nilipoiona picha hii kwa mara ya kwanza, nilicheka sana na kubaki kushangaa udadisi wa hawa nyani. Sasa kama huyu wa mwisho huyu, inaelekea ana kumbukumbu ya kutosha maana ameweza kukumbuka kuwa hii kitu inaenda kichwani na si kwingineko.
Lol. Wacha nikakae nimalizie kicheko