wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, August 01, 2009

TweetThis! Hakuna anayejali: Ajali ya gari yaua 12 Manyara

Hata wiki moja haijaisha!
Sidhani lipo la kusema, na kama lipo, sidhani kama ni wakati muafaka kulisema wakati yaliyosemwa siku za nyuma na Mubelwa, Dr. Faustine, Mimi na wachangiaji wengine, sijasikia wala kuona hatua yoyote madhubuti ikichukuliwa, zaidi tu ya wahusika kusema yale yale ambayo wamekuwa wakiyaema miaka nenda rudi kuwa, "...tutaimarisha ulinzi na sheria za barabarani. Tutawachukulia sheria madereva wazembe na wale waote wanaokiuka kanuni na sheria za matumizi ya barabara" ni kiitikio hata mwendawazimu anakijua. Tangu wameanza kuimba hiyo korasi, hakuna lililorekebika. Wanafanya mambo kwa njia na mtindo ule ule, huku wakitarajia mabadiliko mapya. Ujinga mtupu. Mi nasubiri tu siku wafe wao ndo pengine tuwapate wengine watakaoshughulika, nadhani ndicho kilichobaki.
Saturday, 01 August 2009 16:18
JUMLA ya watu 12 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Fusso Forward walilokuwa wakisafiria kwenda mnadani, kugonga daraja na kupinduka.

Abiria hao walipatwa na ajali hiyo jana majira ya saa tatu asubuhi, wakati wakitokea eneo la Matui kueleka Dosidosi, wilayani Kiteto, Mkoani Manyara.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo, Bw. Habibu Abdalanew alisema kuwa kuwa gari hilo liligonga tuta lililoko karibu na daraja kwenye kona ya kuingilia eneo la mnada wa Dosidosi.

Habari zinasema kuwa gari hilo, ambalo namba zake hazikuweza kupatikana haraka, likiwa katika mwendo wa kasi, liligonga tuta hilo, na kusababisha ajali hiyo.

Baadhi ya majina ya waliokufa katika ajali hiyo ni Shafi Habibu, Mteto Omari, Figo Alan, Msafiri Yahya, Yahaya Ndwata, Mohamed Hassan na mtu moja aliyefahamika kwa jina la Mpemba. Miili ya marehemu na baadhi ya majeruhi wako katika Hospitali ya Kiteto. Majeruhi wa nne walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.

Habari kwa mujibu wa Mohamed Hamad wa: http://www.majira.co.tz

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads