wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, July 26, 2009

TweetThis! Ajali nyingine ya barabarani imeua watu takribani 33

Ninajua fika kuwa jirani yangu Mubelwa Bandio wa blogu ya ChangamotoYetu atakosa kauli kutokana na habari hii kwani ameshaizungumzia mara nyingi kiasi cha kutokwa na povu katika kulizungumzia suala la ajali za barabarani nchini Tanzania.
Dr. Faustine alishaandika kuhusu ajali hizi na kutoa mapendekezo yake, sijui kama kuna mtu aliyasoma hapa au hata kujaribu kumwuuliza ufafanuzi na hatimaye kujaribu kuyatendea kazi. Ni kama dharau vile, il hali watumiaji wa barabara ni sisi na tunaoathirika kwa ajali hizi ni sisi sisi wananchi.
Nilishawahi kuandika kutokana na kusikitishwa na suala la ajali za barabarani, leo wala sina jipya la kusema kwani ni kama vile hakuna anayejali kusaidia kupunguza sababu za makusudi zinazoweza kuchangia ajali hizi kutokea. Si kweli kuwa kila ajali imepangwa kutokea hivyo ilivyo na kwamba hatuna cha kuzuia ajali isitokee. Tukisema hivyo tutakuwa tunajifariji na kukubaliana na ajali zinazotokea kwa uzembe wetu wenyewe. Tutakuwa tunajiongopea nafsi zetu kukiri kuwa ajali hazizuiliki. Ukweli ni kuwa ajali inaweza kuzuilika au kutokuwa na madhara makubwa ikiwa kila mmoja atajali nafasi yake katika kuzuia ajali kutokutokea.
Mathalani:
  1. Mmiliki wa gari kuhakikisha gari lake linapelekwa gereji kabla ya safari ndefu.
  2. Fundi makanika kuhakikisha kuwa anacheki vipuri na hitilafu yoyote katika gari.
  3. Dereva kuhakikisha kuwa anazingatia alama za barabarani na hasa mwendokasi uliopangwa.
  4. Utingo/Tandiboi kuhakikisha kuwa abiria waliopo ndani ya chombo cha kusafiria hawazidi uwezo wa gari na kwamba wapo katika mpangilio kadiri ya muundo wa gari.
  5. Abiria kutokukubali kuswekwa ndani ya chombo cha usafiri kilichokwisha timia idadi ya wasafiri kwani kwa kufanya hivyo, badala ya kuwahi kufika, yaweza kuwahi kufa. Wa kale waliasa, 'kawia ufike'.
  6. Wakandarasi kuhakikisha kuwa barabara zimejengwa katika kiwango stahili na alama za barabarani kutoa maelekezo muafaka kulingana na eneo.
  7. Askari/Usalama barabarani kuhakikisha kuwa wanakagua na kuruhusu chombo kuwemo safarini kwa mujibu wa standadi za usafiri.
  8. Serikali (kitengo husika kama vile mahakama na Wizara) kuwa na sheria za kuwawajibisha watendani katika kila hatua iliyotajwa hapo juu ikiwa kutatokea ukiukwaji wa kanuni na taratibu za usafiri kama zilivyoainishwa na kuelekezwa na wataalamu wetu.
Kwa masikitiko makubwa, inaelezwa na Francis Godwin kwenye blogu yake kuwa:
Habari za kusikitisha ambazo zimenifikia usiku huu nikiwa hapa jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini Bw James Kombe zinadaiwa kuwa zaidi ya abiria 20 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Mohamed Trans wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kupasuka taili na kupinduka likiwa katika mwendo mkali.
Kwa habari zaidi, fuatilia vyombo vya habari na blogu mbalimbali.
The state-owned broadcaster (Tanzania) is reporting that a bus has crashed into a truck in northeastern Tanzania, killing 33 people. Tanzania Broadcasting Corp. is quoting unnamed police officials as saying the accident happened Sunday afternoon in Korogwe, about 210 kilometers (130 miles) northwest of the commercial capital, Dar es Salaam. The bus was traveling to Dar es Salaam from the northwestern town of Arusha, the station reports. Five people remain at the hospital at Korogwe, TBC reports. Other passengers had minor injuries and were discharged from the hospital after being treated, the station says. Buses are Tanzania's main public transport between towns and many bus drivers exceed the speed limit.
News source: http://www.chron.com/disp/story.mpl/ap/world/6548115.html

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads