wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, February 01, 2009

TweetThis! Video : Ajali ya kutisha iliyotokea Arusha mwezi Januari 2009

Ajali zinazotokea Tanzania zinazuilika ikiwa sheria zinazotungwa zitasimamiwa na ikiwa heshima ya utii wa sheria itazingatiwa kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake. Hivi, kila mmoja akitimiza wajibu wake, hizi ajali hazitapungua?
Tuseme,
  • Raia ajue haki na wajibu wake na afanye inavyotakiwa.
  • Mmiliki wa vyombo vya usafiri naye ajue wajibu wake na autekeleze.
  • Vitengo vyote vya Serikali vinavyohusika na vyombo vya usafiri, sheria za usafiri pamoja na miundombinu vifanye kazi yake.
Suala la ajali litakuwa la kuzungumziwa?

Hii video inasikitisha sana, ni ajali iliyotokea mjini Arusha mwishoni mwa mwezi jana mwaka huu.

1 feedback :

Mzee wa Changamoto said... Sun Feb 01, 07:10:00 PM MST  

Dada. Nimechoka na naamini wengi wamechoshwa na hizi ajali. Tumechoshwa na salamu za rambirambi. Lakini pia swali hapa ni kuwa nani wa kulaumiwa na nania anachukuliwa hatua? Inasikitisha kuona kuwa upo uwezekano mkubwa wa waliojeruhiwa kutoiona haki yao licha ya maumivu na hata ulemavu uliowapata kuwaharibia utendaji kazi wao wa kila siku. Nasema hivi kwa kuwa nimekutwa na dhahama hii mwaka 1999 na mpaka mwaka jana nimekuwa nikihudhuria therapies na hakuna niliyesikia alisaidiwa japo gharama za matibabu. Nailaumu saana serikali kwa kutokuwa makini katika hili. Katika kuhakikisha waliojeruhiwa (na ambao wakati mwingine wanatembelewa na viongozi wa juu wa nchi wanapokuwa hospitali)wanapata haki yao ya "kusaidiwa" gharama za matibabu. Niliwahi kuandika siku mbili kabla ya XMas nilipikuwa nakumbuka miaka 9 tangu nipate ajali hiyo (http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/12/kila-penye-raha-pana-uwezekano-wa.html) kuwaomba madereva kuwa makini hasa nyakati za sikukuu, lakini nadhani sasa imezidi. Ndio maana kwenye blog yangu niliandika juu ya kuchoshwa kwa hizi salamu za rambirambi toka kwa wakuu wa serikali wenye dhamana ya kulinda maisha yetu lakini HAWATAKI kufanya hivyo kwa sababu zao binafsi. http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/tumechoshwa-na-salamu-za-rambirambi-na.html

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads