wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, July 12, 2009

TweetThis! Taarifa na Fomu ya kusajili simu yako toka TCRA

Ili kujipatia nakala ya Tangazo na Fomu, bofya hapa kuipakua  (pdf) kutoka TCRA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA
USAJILI WA SIMU ZA MKONONI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inawajulisha wananchi kuwa kuanzia tarehe 1 Julai 2009 makampuni yote ya simu za mikononi yataanza kusajili wateja wao waliopo na wapya ili kuhakiki umiliki wa namba za simu wanazozitumia. Zoezi hili litaendelea kwa miezi sita hadi tarehe 31 Desemba 2009.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inawahimiza wananchi kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo ambavo yametayarishwa kwa mfumo wa maswali na majibu.

1. Swali: Kwa nini usajili namba ya simu?
Jibu: Kwa ajili ya kukulinda wewe na namba yako dhidhi ya matumizi mabaya ya simu.

2. Swali: Kitambulisho cha aina gani kitahitajika wakati wa usajili?
Jibu: Ili uweze kusajiliwa unahitaji kufika kwenye ofisi ya kampuni yako ya simu au wakala wake na moja ya vitambulisho vifuatavyo ambapo utawapatia kivuli chake:-

(i) Kitambulisho cha mpiga kura
(ii) Pasipoti
(iii) Kitambulisho cha mfuko wa pensheni
(iv) Leseni ya udereva
(v) Kitambulisho cha SACCOS
(vi) Kitambulisho cha benki
(vii) Kitambulisho cha ajira pamoja na barua ya mwajiri
(viii) Kitambulisho cha chuo cha elimu ya juu
(ix) Kitambulisho cha uanachama kwenye kilabu
(x) Barua ya serikali za mitaa ikiwa na picha, sahihi na muhuri

3. Swali: Nisipojisajili ifikapo tarehe 31Desemba, 2009 nini kitatokea?
Jibu: Namba yako itafungwa ili usiweze kuitumia kwenye mtandao wa simu nchini Tanzania.

4. Swali: Nani na wapi ninaweza kusajili namba yangu ya simu?
Jibu: Unaweza kusajiliwa na kampuni yako ya simu za mkononi au mawakala wao waliopo sehemu mbali mbali nchini.

5. Swali: namba ngapi za simu (simcard) ambazo ninaweza/ninaruhusiwa kusajili?
Jibu: Idadi yoyote kadri utakavyo.

7. Swali: Kuna uhakika gani wa usiri wa taarifa zangu nitakazotoa kwa kampuni ya simu za mkononi au wakala wao?
Jibu: Kampuni zote za simu nchini zinawajibika kwa mujibu wa sheria, kutunza taarifa za wateja wao ikiwa ni pamoja na taarifa za matumizi.

8. Swali: Taarifa zipi zinahitajika wakati wa usajili?
Jibu: Tafadhali angalia mfaano wa fomuya usajili hapo chini:-

Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

SIM Card Registration Form

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads