...siyo kila mtu aje mbugani kujenga hoteli - J.Kikwete
Habari kutoka gazeti tando la Mwananchi
RAIS Jakaya Kikwete amepinga hoja ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa aliyoitoa bungeni enzi za uongozi wake ya kutaka zijengwe hoteli nyingi maeneo ya hifadhi za taifa. Badala yake Rais Kikwete ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha kuwa inadhibiti ujenzi holela wa hoteli katika maeneo ya mbuga za wanyama.
Akizungumza wakaki wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Bilila Kempinski yenye hadhi ya nyota tano katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, Rais Kikwete alisema kama kutakuwepo na ujenzi holela wa hotel katika mbuga baadaye kunaweza kuleta athari kwa wanyama. “Tunahitaji hoteli nzuri za kitalii zenye sifa na siyo kila mtu aje mbugani kujenga hoteli. Haitaleta maana yeyote, hivyo nawagiza ninyi TANAPA (Shirika la Hifadhi la Taifa) na wizara husika kusimamia vyema jambo hili,” alisema Kikwete.
Mwaka 2007, Lowasa aliwahi kulieleza bunge kuwa serikali inakusudia kuanza kujenga hoteli kwa wingi katika maeneo ya mbugani kwa lengo la kuvutia watalii kutokana na ukosefu wa hoteli zenye hadhi nchini. Alisema sekta ya utalii ni eneo muhimu katika ukuaji wa uchumi hapa nchini kwani katika kipindi cha mwaka 2007/2008 sekta hiyo iliweza kuchangia pato la taifa kwa asilimia 17.2 na kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 25, jambo ambalo halikuwahi kutokea huko nyuma.
Alisema kukamilika kwa hotel hiyo ni sehemu ya kutangaza utalii katika mbuga ya Serengeti nje ya nchi, hivyo ni vema wamiliki na wafanyakazi katika hotel hiyo wakafanya kazi kwa uaminifu ili kuvutia zaidi wawekezaji. “Tutapokea watalii wengi katika hoteli hii, lakini hata sisi tumepata ajira kutokana na kukamilika kwa hoteli hii, msiiharibu, ipendeni ili nayo iendelee kuwalea,” alisema Rais Kikwete.
Alisema hivi sasa Serikali ipo katika mchakato wa kupunguza kiwango cha malipo kwa hati ya kusafiria kwa watalii kutoka asilimia 100 hadi kufikia 50 kwa mtalii mmoja, lengo likiwa ni kuondoa vikwanzo vinavyosababisha kupungua kwa watalii nchini hasa katika kipuindi hiki cha kuyumba kwa uchumi duniani.
2 feedback :
Yeah right. POLITRIX
Dada Subi,namponeza rais wetu Dr.J K Kikwete kwa msimamo wake huo, kweli inaonyesha jinsi ambavyo muheshimiwa naafanya kazi kwa uwazi,kinaco takiwa kwetu sisi ni kufuata ushauri wa rais kufanya kazi kwa bidii na uaminifu,ili tuweze kulinda ajira zetu.Ajira ngumu kwa kipindi hiki msukosuko(kudolola kwa uchumi).
HEKO RAIS KIKWETE