wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, July 21, 2009

TweetThis! Hii kali, eti Wazungu wanaiba fedha kupitia ATM za Bongo

Kwa mujibu wa taarifa za habari kupitia magazeti ya Mwananchi na HabariLeo, yaah, habari ndo hiyo hapo chini!
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata raia wawili wa Bulgaria wanaodaiwa kuiba zaidi ya sh milioni 70 katika mashine za kutolea fedha, ATM jijini Dar es Salaam. Watuhumiwa hao, Nedko Stanchen (34) na Stella Nedekcheva (23) walikamatwa mwishoni mwa wiki jijini humo baada ya polisi kuweka mtego wakishirikiana na benki ya Barclays wilayani Kinondoni.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova amesema leo kuwa, vijana hao wanadaiwa kuhusika katika mtandao wa wizi wa fedha katika mashine za ATM za benki mbalimbali. Amesema, polisi waliweka mtego baada ya mfanyakazi wa benki ya Barclays kugundua kuwa kuna vifaaa vilikuwa vimewekwa katika mashine za ATM. Amewaeleza waandishi wa habari kuwa, mfanyakazi huyo alikuwa anafanya usafi, na kwa mujibu wa Kova, vifaa vilivyowekwa kwenye mashine za ATM ni kamera na kifaa cha kunakili taarifa za wateja zilizomo kwenye kadi za ATM. Kwa mujibu wa Polisi, watuhumiwa hao wameiba fedha katika mashine za ATM za benki tofauti, na wamekutwa na kadi tano za ATM za benki ya Barclays, Stanbic na vifaa mbalimbali vya mtandao huo wa wizi.

“Hawa watuhumiwa waliweza kuja na mbinu yao ambayo nahisi kuwa ni ya muda mrefu tangu waanze kuitumia tayari fedha nyingi zimeibwa, tumewakamata na vifaa maalumu vyenye uwezo wa kunakili taarifa za wateja toka katika kadi zao za ATM na hivyo kuwarahisishia kuchota fedha toka katika Mashine hizo na baada ya kubaini hilo tuliweka mtego mara moja na kufanikiwa kuwakamata” amesema Kova.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads