wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, June 03, 2009

TweetThis! Video: Mengi ataendelea na vita dhidi ya ufisadi

Niseme kwa kauli yangu kuwa, vita dhidi ya ufisadi si ya mtu mmoja wala kikundi fulani cha watu, ni vita ya wananchi wenye uchungu na hasira dhidi ya dhuluma na mienendo isiyo sawa. Itikadi na tofauti katika mambo kadhaa ni hulka ya ubinadamu lakini pia katika tofauti hizo, yapo mambo ya msingi ambayo hatupaswi kuyafumbia macho kwa sababu za tofauti zetu zisizotusaidia kwa namna yoyote ile.
Aliye na vielelezo juu ya wizi na ubadhirifu wa mali ya umma apeleke nakala kwenye mamlaka husika na mamlaka hiyo itupatiee ukweli wa usahihi wa mambo kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
Atakayebainika kupotosha na kuongopa kwa makusudi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Atakayefichuka kuhusuka na shutuma pamoja na tuhuma husika, ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Hatutaendelea hata kidogo kwa kutokuwa na soni au nia thabiti ya kuzuia ubadhirifu.
Yana mwisho!, ila mwisho wake utakkuwa mzuri au mbaya? tutajua siku hiyo itakapofika.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads