wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, June 09, 2009

TweetThis! Ajali yaua 6 na kujeruhi 37 - basi la Hajji's ya Dodoma

Watu sita wamekufa papo hapo na wengine 37 kujeruhiwa baada ya basi la Hajji's walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la mbele la upande wa kulia na kupinduka.

Ajali ililihusisha basi la Hajji’s aina ya Scania namba T441 AYN, ilitokea siku ya Jumatatu saa 5:45 asubuhi katika eneo la Mtumba kilomita 20 kabla ya kufika mjini Dodoma, likitoka Dar es Salaam kwenda Singida.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dk. Geodfrey Mtey alisema alipigiwa simu saa sita kasoro robo kuwa ajali imetokea maeneo ya Mtumba na ilipofika saa 6 mchana walianza kupokea majeruhi ambao jumla yao ilitimu majeruhi 37 ambapo 19 kati yao walitibiwa na kuondoka. Kati ya majeruhi hao, mmoja kati yao ana hali mbaya ambapo amekatika mkono wake wa kulia.

Dt Mtey aliwataja majeruhi waliolazwa kuwa ni pamoja na watoto wawili wa familia moja ambao ni Yakob Daniel na Ezekiel Daniel, Bw. Idi Mussa, Bw.Hassan Kambina Bw. Ali Mbegu ambao wote wamelazwa Wodi namba moja katika hosptali ya mkoa.

Majeruhi ni pamoja na Bi.Hamida Ramadhani, Bw.Agnes Blezi, Bi. Belitha Lucas, Bi.Mwanaidi Kisoja, Bi. Amina Hussein, Bi. Rehema Hassan, Bi.Costancia Ngole, Bi.Lidya Athman naBi. Juliana Leonard ambao wamelazwa wodi namba kumi.

Waliolazwa katika wodi namba nane ni Bi.Rozania Blezi Sukwi na Bi.Rithwat Abdul.

Waliofariki walikuwa akiwasubiri ndugu, kwenda kuwatambua.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bw. Omar Mganga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi upande wa dereva. Dereva wa gari hilo Daud John alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo na jeshi la polisi linamtafuta.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads