wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, May 30, 2009

TweetThis! Makulilo akamilisha ubalozi Marshall Uni. kesho yu safarini kuelekea Tanzania

Bloga na aliyekuwa balozi wa Tanzania huko Marshall University katika mwaka wa masomo 2008/2009 Makuliko Jr ametuma salama za kuaga akisema:
Da Subi
Kesho nitaondoka, nitakua safarini kuelekea Dar. Nimemaliza mkataba wangu wa kufundisha mambo ya utamaduni hapa Marshall University. Hivyo ninakwenda Tanzania, nitaandaa ile scholarship workshop...nitakujulisha mambo yakiwa tayari kabisa. Then nitarudi marekani mwezi August katikati kwa ajili ya Masters Studies at University of San Diego, California kwa ajili ya Peace and Justice Studies.
Nashukuru kwa ushirikiano wako Dada. Mungu azidi kukupa nguvu ya kuweza kuhakikisha watu wengi zaidi wananufaika na uwepo wako duniani.
Nitakua in touch daima.
-----------------------------------------------------------
Ernest Boniface Makulilo
Graduate Student
MA - Peace and Justice Studies
The Joan B. Kroc School of Peace Studies
University of San Diego, California
Blog www.makulilo.blogspot.com
-------------------------------------------------------------
Ambao niliujibu hivi:
Hongera sana Makuliko kwa kukamilisha mkataba wako vyema na Marshall University. Umekuwa balozi mzuri na umetumia nafasi yako vyema katika kuwasiliana na watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, zaidi sana umekuwa mwanga na msaada kwa watu waliokutaka ushauri kuhusu jambo hili na lile.
Nimejifunza mengi toka kwako, nimepata mema mengi ya kuzingatia kutoka kwako, yote yamekuwa heri tangu tumefahamiana.
Ni matarajio yangu basi kuwa utakaporejea Tanzania na kukamilisha Workshop ya Scholarship, wengi zaidi watahamasika na kuitumia intaneti kwa manufaa zaidi katika maisha.
Ninakuombea safari ya salama na ufikapo huko utukumbuke.
Mwenyezi Mungu mwingi wa baraka awe pamoja nawe!
.end.
Subi

2 feedback :

Anonymous said... Sun May 31, 07:26:00 AM MST  

Twamkaribisha Makulilo Bongo na asafiri salama. Nawe subi pongezi kwa unayoyafanya kwa sasa. mungu akubariki
Hamis

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads