wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, May 13, 2009

TweetThis! Kisiwa cha Migingo katika ziwa Nyanza (Victoria)

Jana katika taarifa ya BBC Swahili (Dira ya Dunia), alisikika raisi wa Uganda, mhe. Yoweri Museveni akisema kuwa, 'ni kweli kwamba kisiwa cha Migingo kipo katika eneo la Kenya lakini, maji yanayozunguka Kisiwa hicho yapo sehemu ya Uganda'.
Haya, mi sielewi tena Jografia ikishaingiliwa na Siasa maana ni vurugu tupu na matokeo yake ni wananchi kutaabika tu.

Chanzo cha ugomvi huu si juu ya, ni nani ndiye mmiliki wa kisiwa? bali, ni nani mwenye ruhusa kamili ya kuvua samaki humo? ("mapanki" - Nile Perch kama unakumbuka ile documentary film ya Hubert Sauper).

Tayari nchi hizo mbili zimeunda tume ya pamoja ya kushughulikia suala hili, wananchi wakisubiri matokeo.
Kinachochunguzwa zaidi kwa wakati huu ili kung'amua ukweli ni je, kisiwa hicho kipo Mashariki au Magharibi mwa kisiwa kingine kidogo cha Pyramid ambacho ni dira kwa mujibu wa katiba ya nchi zote mbili. (Tanzania katiba yetu ipo wapi? siku ikihitajika tusijeumauma vidole na midomo bure, ohooo).
Kwa mujibu wa dira hiyo, ikiwa rasi ya Migingo itaangukia Magharibi mwa mstari utakaochorwa kutoka kisiwani Pyramid kuelekea Kaskazinibasi kisiwa cha Migingo kitakuwa mali ya Uganda na ikiwa kinyume cha hapo basi itakuwa ni mali ya Kenya.

Kisiwa chenyewe kina ukubwa wa kadiri ya nusu ya eneo la kiwanja cha mpira wa miguu tena inawezekana kabisa kuwa kilikuwa kimezama ndani ya maji mengi ya ziwa Nyanza (Victoria) hadi miaka ya tisini kilipoanza kuonekana kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika ziwa hilo. Inaaminika kuwa wavuvi wa kwanza kuishi kisiwani hapo walikuwa wa asili ya Kenya na walifika hapo mnamo mwakawa 1991 baada ya hapo inaripotiwa na WaGanda kuwa mvuvi kutoka Uganda alifika kisiwani hapo mwaka 2004 na hakukuta mtu yeyote. Hadi sasa idadi ya wakazi wa Migingo inakadiriwa kuwa ni  kiasi cha watu elfu moja.
Ramani unayoiona huenda ikabadilika baada ya siku chache ikiwa yatakuwepo makubaliano baina ya WaKenya na WaGanda kuhusu ni nani hasa aliye mmiliki wa kweli wa Kisiwa cha Migingo. Ramani hii imechorwa na bwana "amproehl" kufuatia maelezo ya katiba ambayo yanaegemea upande wa Kenya.
view photospicture uploaded on Flickr on May 12, 2009
by amproehl

1 feedback :

Yasinta Ngonyani said... Wed May 13, 03:14:00 AM MST  

Subi, kweli hii ni vurugu tupo. Au twaweza kusema huu ndio mwanzo wa kuanza vita pia

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads