wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, May 18, 2009

TweetThis! Ajali mkoani Arusha yaua wa5 papo hapo

Ajali iliyotokea jana saa 12 as. eneo la Usa River mkoani Arusha iliyolihusisha lori aina ya Scania lenye namba KBH 742C la Kenya na Toyota Land cruiser yenye namba T366 AJL iliyokuwa imebeba  wafanyakazi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Tanzanite ya Tanzanite One ya mkoani hapo imesababisha watu 5 kupoteza uhai papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Bw. Basilio Matei, amethibitisha kutokea ajali hiyo kwa kusema kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa Scania iliyokuwa imebeba maua ikiendeshwa na Hamis Maulid aliyekuwa anajaribu kuyapita magari mawili yaliyokuwa mbele yake.

"Huyu dereva wa Scania ndiye chanzo cha ajali wakati alipokuwa 'aki- overtake. Alikuwa akitokea Moshi kuja Arusha, ndipo alikutana uso kwa uso na Toyota Land Cruiser iliyokuwa ikitokea Arusha kuelekea Mererani kwenye machimbo ya Tanzanite' - Matei.

Majeruhi walipelekwa Hospitali za Selian na Mount Meru kwa matibabu zaidi.

Waliokufa ambao wote walikuwa ni wafanyakazi wa Tanzanite One wametwajwa kuwa ni:
  1. Bw. Mathayo Mushi (32) mkazi wa Sakina na dereva wa Toyota Land Cruiser.
  2. Bw. Judica Mollel
  3. Bw. Omar Makuka (36) mkazi wa Majengo
  4. Bw. Uswege Mwapanga (27) mkazi wa Sakina
  5. Bw. Frank Mwakatobe (33) mkazi wa Sakina
Majeruhi na ambao ni wafanyakazi wa Tanzanite One ni:
  1. Bw. Boni Mutaba (28) mkazi wa Ngaramtoni
  2. Bw. Daimoni Kingdom (34) mkazi wa Majengo
  3. Jacob Peter (27)
  4. Bw.Lucas Massawe( 30) mkazi wa Sanawari
  5. Bw.David Makame mkazi wa Sombetini
  6. Bw. Gideon Zacharia (33) mkazi wa Sakina
  7. Bw. Amani Julius (25) mkazi wa Kambi ya Fisi
  8. Bw. Mtunigwa Mwaibuja (35)
  9. Bw. Desder Mbowe (32) mkazi wa Sakina.
Pole kwa wafiwa na kwa ndugu, jamaa na rafiki wa marehemu. Mwenyezi Mungu awapumzishe pema.
Afya njema na nguvu tena kwa waliojeruhiwa katika ajali. Ugueni pole!

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads