wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, March 11, 2009

TweetThis! Mfalme yu katika himaya yake, bishaga mahodi!

Sasa mtu kama huyuuu, mkiwa pamoja, na wewe ndiye unapiga hiyo picha, unamwambia mwenzio 'simba'? ama unapata kigugumizi cha kukaba koo? ama unanyoosha mkono huku miguu inakutetemeka usijue la kusema? ama unatupa kamera na kuanza kutimua kusikoeleweka? ama unapiga goti kwa kulegea? ama unalia? au unapanda mtini?
Yaani, hapa unazungumzaje na simba na kumwomba akuelewe? Bofya hiyo picha kuikuza ujionee kimbembe.
Jama eeh, ukiingiaga maeneo ya wenyewe ujifunzage masiri ya urembo. Sheria kama vile za kuvuka barabara, kwanza angalia kushoto, pili, pili angalia kulia, tena, tena angalia kushoto vuka barabara! na hapo ni uwe unatembea upande wa kulia mwa barabara unatizamana na magari na si magari nyuma yako kwenye nchi zinazoendeshea mkono wa kulia na vice versa kwa nchi za LHD.

4 feedback :

Martin said... Wed Mar 11, 11:53:00 AM MST  

dah kitoweo saaaafi kabisa kwa simba huyu leo!!!
nini kilitokea sasa...alikamatwa? au alisave?

Subi Nukta said... Wed Mar 11, 06:44:00 PM MST  

Hapo pagumu kufahamu mwisho wa "hadithi" hii ulikuwaje. :-E

Bongosamurai said... Thu Mar 12, 06:36:00 AM MST  

Hapa ni kutimua mbio mpaka soksi ivuke na kiatu kubaki mguuni!

Subi Nukta said... Thu Mar 12, 01:02:00 PM MST  

Hizo mbio za kuvukwa soksi na kiatu kubakia mguuni lazima zimetokana na zile mbinu za sketi kubanana skin tight ikapwaya! kazi ipo nhe he :-D

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads