wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, March 31, 2009

TweetThis! Mamia ya WaTanzania wafurika kusali na kumpokea Fredrick Sumaye

Reading - UK.
Mamia ya WaTanzania waishio Reading Uingereza jana walifurika katika misa ya Kiswahili iliyoendeshwa na Mama Mchungaji Tumaini Kalaghe wa dhehebu la Kilutheri la hapa mjini Reading.

Aidha, katika ukumbi uliofurika watu wa madhehebu mbalimbali hadi yale yasiyo ya KiKristo, ulijawa na hamasa ya Umoja wa Kitanzania na shauku ya kumsabahi Waziri Mkuu Msaafu aliyesafiri kwa treni toka London hadi Reading akiambatana na mkewe Mama Esther Sumaye.

Sumaye alishiriki kikamilifu katika misa hiyo na alitoa salam za kizalendo kuwathibitishia WaTanzania hao kuwa Serikali ya Kikwete inastahili pongezi kwa kuwa na vigezo vyote vya kujenga utawala bora wa kisheria katika kuinua maisha ya MTanzania.

Pia, kwamba Raisi Kikwete ametoa uhakika wa nchi yetu kuwa Serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa hakuna MTanzania atakayekufa kwa njaa hasa wakati huu wa matatizo ya uchumi duniani. Sumaye alisisitiza (huku akishangiliwa na ukumbi mzima) kuwa Raisi anafanya kazi nzuri na wazi na anastahili kuungwa mkono wa WaTanzania wote.

Mhe. Sumaye aliwaasa WaTanzania wote walioko nje ya nchi kuongeza bidii katika shughuil zao na kidogo wakipatacho kujitahisi kuwekeza nchini. Baadaye Sumaye alitembelea The Kilimanjaro Restaurant ya kisasa, iliyoko Oxford Rd. inayohudumia vyakula vya KiTanzania ambapo yeye na ujumbe wake walipata mlo na WaTanzania wengine.

Ndugu Sumaye aliwashukuru WaLutheri, CCM na Jumuiya ya WaTanzania kwa kushiriki naye.

Taarifa hii imeandaliwa na Tanzania Association Reading.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads