wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, March 08, 2009

TweetThis! CHAN 2009 Final : Congo DRC 2 Ghana 0

I do not have the full match recorded but only the second half a few minutes after the kickoff until the end of celebrations at the stadium. I couldn't upload it here because of the MB limits and uploading it in google did not produce good results as the recording resolution was small and changing it from .avi format to .mwv the video lost some quality. Sorry about that. If you still want it, drop me I line and I will see what I can do. Use this link to download the video: veoh.com - CHAN 2009 Congo DRV vs Ghana.

LIVE updates
Wamesali pale uwanjani kwa mfano wa wanavyosali 'walokole'.
KONGO DRC ndiye mshindi wa kombe la CHAN 2009.

Hadi mwisho wa mechi Kongo DRC 2 Ghana 0.
  • Vituko vya kipa wa Kongo DRC vimeendelea hadi kawaambukiza wachezaji. Baada ya mechi kipa na wachezaji wake wamecheza kwa staili ya kufagia uwanja kwa makalio, hii staili ni mpya kabisa kuiona. Nderemo zina mashangilio yasiyo na fomula.
  • Kama Brazili wanacheza Samba Soccer basi Kongo DRC wanacheza Lingala Soccer!
  • Kongo DRC wanacheza kabumbu la kuridhika kweli na kandanda yao safi, wanaonana vyema kwenye pasi.
  • Mechi ninaiona live pia kupitia http://tv.abidjan.net/
  • Kongo DRC 2 Ghana 0
  • Kuna vituko uwanjani huko, kipa anacheza ngoma kwa makalio baada ya goli kufungwa, mithili ya kufagia uwanja kwa makalio, ha ha haa
  • Samahani sana, kwa sababu zilizopo nje ya uwezo wa security zone and restriction za myafricanfootball haiwezekani ku-embed link na ndiyo maana video haioneshi picha. Samahani sana.
  • Dakika ya kwanza tu ya kipindi cha pili, goli safi la kichwa baada ya pasi toka mpira uliochongwa kwenye kona unatinga nyavuni na kuwaweka mbele Congo DRC 1 Ghana 0.
  • Hadi kipindi cha kwanza kinaisha, Kongo DRC 0 Ghana 0
  • Thank to Malkiory Matiya for the access code to the live match!

6 feedback :

Subi Nukta said... Sun Mar 08, 11:28:00 AM MST  

Nilikuwa sijui kama itakuwepo mechi kati ya watani wetu wa jadi na Tunisia, basi kunako majaaliwa nikiipata linki nitaiposti.

Subi Nukta said... Sun Mar 08, 11:30:00 AM MST  

Hapa nina video, nimerekodi katikati ya kipindi cha pili najaribu kui-upload angalao mpate uhondo wa kabumbu na goli la pili na vimbwanga vya kipa na hatimaye kukabidhiwa kombe na mwishowe highlights za mechi nzima.

malkiory said... Sun Mar 08, 12:08:00 PM MST  

Hello Subi, endeleza huo moyo huu wa kuwajali na bidanadamu wengine. Sasa tusubiri tarehe 28.3.09 kati ya watani wetu wa jadi na Tunisia.

Martin said... Mon Mar 09, 07:52:00 AM MST  

hi dada subi. Martin Manchester hapa!
nadhani mechi ya YANGA na AL AHLY ya msri itaonyeshwa sababu waarabu hawako nyuma katika hilo. je unaweza kujitahidi kuipata hiyo??? na sijui kwa sisi wa UK tutaiona muda gani. tutashukuru sana mungu akubariki!!
martin
manchester, Uk

Subi Nukta said... Mon Mar 09, 09:59:00 AM MST  

Martin, dah, wala sikuwa najua kama hiyo mechi ipo, sasa nimejua zitakipiga uwanjani tarehe 15 Machi, yaani Jumapili, nitatafuta linki huko kwa MaFarao. Asante kwa kunistua! 8-)

martin said... Mon Mar 09, 11:01:00 AM MST  

i appreciate. ok thanks and lt's wait ot see that you succeed in that
martin

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads