wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, February 23, 2009

TweetThis! Jinsi ya kuweka audio/video kwenye blogu/tovuti kutumia WMP

WMP = Windows Media Player
Hii ni njia ya kuweka video/audio ambayo haipatikani kwenye tovuti zinazokupa 'embed code' kama vile YouTube, iMeem, GoogleVideo, LiveLeak nk.

ZINGATIA: Huwezi kuweka video au audio kutoka kwenye kompyuta yako, unahitajii kuwa na URL ya mahali ambapo video ama audio imehifadhiwa ama kuwa na hosting kama ni audio/video zako mwenyewe.
URL ya video huwa inaishia na .wmv au .asf au .asx nk
URL ya audio huwa inashia na .mp3 au .wav

Tumia sehemu ya 'Edit HTML' (badala ya 'Compose') wakati wa kuandaa posti yako unayotaka kuweka audio kwani utatumia code ambayo inasomeka kwenye HTML na kisha kubadilishwa kuwa kwenye pleya.

Hapa ninaweka code mbili yenye 'control' muhimu tu (badala ya code ndefu ambayo inaweza kukuchanganya bure).

Code fupi kabisa kwa ajili ya audio:
<embed type="application/x-mplayer2" pluginspage="http://www.microsoft.com/windows/windowsmedia/download/"
src="FUTA-HAPA-NA-WEKA-URL-YA-VIDEO-AU-AUDIO-YAKO"
Name=MediaPlayer ShowControls=1 ShowDisplay=0 AutoStart=0 ShowStatusBar=0 width=200 height=70></embed>
Code ndefu kidogo ya audio na video:
<object id="MediaPlayer" width="557" height="313" classid="CLSID:22D6F312-B0F6-11D0-94AB-0080C74C7E95"
standby="Loading Windows Media Player components..." type="application/x-oleobject">
<param name="FileName" value="FUTA-HAPA-NA-WEKA-URL-YA-VIDEO-AU-AUDIO-YAKO">
<param name="Autostart" value="false">
<param name="ShowControls" value="true">
<param name="ShowDisplay" value="false">
<param name="ShowStatusBar" value="false">
<param name="ShowTracker" value="false">
<param name="Volume" value="0">
<embed type="application/x-mplayer2" src="FUTA-HAPA-NA-WEKA-URL-YA-VIDEO-AU-AUDIO-YAKO" name="MediaPlayer"
width="557" height="313" Autostart="0" ShowControls="1" ShowDisplay="0" ShowStatusBar="0" ShowTracker="0" Volume="0"></embed></object>

Unaweza kubadilisha urefu (height) na upana (width) kadiri unavyotaka hasa kama unatumia audio na hupendi sehemu ya juu iwepo basi punguza (height).

Unaweza pia kubadilisha maneno au tarakimu zilizomo kwenye sentensi zinazoanza na neno 'param....'. Kwa mafano, kama hutaki audio/video icheze moja kwa moja mtu anapofungua ukurasa, basi unaweza kubadilisha badala ya 'autostart' kuwa 'true' ondoa neno 'true' na weka 'false' hivyo mtu akifungua ukurasa huo atakuwa na uchaguzi kama asikilize ama la. Au, badala ya 'true' na 'false' unaweza kubadili penye tarakimu '1' ukaweka '0' na vice versa.

Endelea kuchokonoa zilizobakia kadiri unavyotaka na utaona mabadiliko yake, ikiwa huyapendi unaweza kuyabadili kadiri ya uchaguzi wako.

Hiyo ndiyo siri walinayoitumia baadhi ya watu wenye totuvi zenye miziki wengine huwa wanaacha control uamue kuzima ama kuacha iimbe wakati wengine huwa wanaficha control na kupunguza ukubwa wa pleya kukunyima usiwe na uchaguzi wowote.

Hii ndiyo njia niliyoitumia kuweka pleya ya TV ya kutizama CHAN na redio mbalimbali kwenye tovuti ya nukta77.com

Mfano wa code ya kwanza (audio pekee)
Nimetumia code ya audio kama ilivyo na kuweka URL ya audio "Barua kwa Yakobo"

Mfano wa code ya pili (audio/video)
Nimetumia code ya audio/video nikabadili width kuwa 300 wakati height nimeifanya 200 kisha URL na kuweka audio clip ya wimbo wa mpiga saxophon Jackiem Joyner - ya wimbo I am waiting for you' http://www.fileden.com/files/2006/12/19/531659/128.mp3 pleya ikawa:

Hakikisha kuwa kwenye audio code usisahau alama za code za kufungua <embed> na kufunga </embed> Na kwenye audio/video ziwepo za kufungua <object na kufunga </object>
Ukizikosea hizo, posti yako itakataa ku-publish na kila mara utapata error message ikikutaka urekebishe kitu kwenye code ya pleya hiyo. Pia hakikisha URL yako imekamilika na umeibandika mara moja tu kwenye audio code wakati kwenye audio/video code uibandike mara mbili.

Maneno 'embed' na 'object' ingawaje yote hufanya kazi moja, mara nyingi huwa yanatumiwa kwa pamoja ili kusaidiana katika browsers tofauti kwani browser mfano Internet Explorer ina maringo sana, ikipatwa na wazimu huwa inadai 'object' ndipo ioneshe pleya, Firefox nayo inaweza kudengua kidogo ikadai 'embed' ili ioneshe pleya ndiyo maana ni bora kuzibandika maneno yote mawili ili kuvunja kidomodomo na maringo ya browsers.

Kwa kawaida watu wengine huwa wanasema ukoko ni mtamu kuliko ugali wenyewe, mimi ni mmoja wao, ndiyo maana nimeacha mstari huu wa mwisho makusudi. Ikiwa nimekuzeveza sana na maelezo hapo juu, basi tumia short cut hii: Automatic WMP code generator

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads