Bibi Sarah Obama kuhudhuria maapisho ya mjukuu Barack Obama

Bibi Obama atakuwa mmoja wa wageni wa heshima na ataongozana na ujumbe maalum kutoka katika serikali ya Kenya, Umoja wa Afrika na wanadiplomasia wengine watakaopewa fursa ya kushiriki tafrija maalumu siku moja kabla ya tarehe ya kuapishwa Barack Obama kama raisi wa 44 wa Marekani. Waziri wa mambo ya nje wa Kenya pamoja na kikundi cha kwaya cha 'Boys Choir of Kenya' nao watasafiri kujumuika katika mwaliko huo utakaofanyika katika hoteli iliyopo mjini Washington.

Kwenye kitabu chache cha "Dreams from My Father", Barack anaeleza kuwa alikutana na kusabahiana na bibi yake (Sarah) kwa mara ya kwanza mwaka 1988. Ingawaje ilikuwa ni vigumu kuelewana lugha, bado waliweza kufahamiana katika mambo kadhaa. Obama katika kitabu chake hicho anaandika,
Our mutual vocabulary exhausted, we stared ruefully down at the dirt until (half-sister) Auma finally returned".
...and Granny then turned to Auma and said, in a tone I could understand, that it pained her not to be able to speak to the son of her son.

Kabla ya safari hii, Sarah Obama amewahi kuitembelea nchi ya Marekani mara mbili.
Ninamtakia safari njema yenye furaha za shamra shamra na sherehe za kuapishwa mjukuu wake kwa hatua na mafanikio aliyoyafikia hadi sasa (na pengine baadaye).
0 feedback :